
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba leo Desemba 21, 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Lindi-Ruangwa- Nachingwea, katika kijiji cha Chimbila A wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Mradi huo wa maji kutoka Mto Nyangao uliopo Wilaya ya Lindi, unatekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa mazingira vijijini (RUWASA), na utanufaisha vijiji 56 katika Wilaya za Ruangwa (vijiji 34), Wilaya ya Nachingwea (vijiji 21) na Wilaya ya Lindi (Kijiji 1).
Mradi huo utagharimi kiasi cha shilingi Bilioni 119 na mpaka sasa ujenzi wake umefikia asilimia 67% ya utekelezaji.
Mradi huo umeanza utekelezaji February 2023 na unatarajiwa kukamilika June 2026 kwa hatua ya kwanza. Hata hivyo ifikapo February 2026 baadhi ya vijiji vitaanza kupata huduma ya Maji.
Akizungumza baada ya uzinduzi huo, Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ameridhishwa na hatua ya utekelezaji wa mradi ambayo imefikiwa.
“Hivi ndivyo Rais Dkt. Samia anataka kuona namna kazi inavyofanyika. Hapa tumeona asilimia ya utekelezaji ni kubwa kuliko fedha zilizotolewa hadi sasa”
Mheshimiwa Dkt. Mwigulu ametumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa kwa kuasisi mradi huo na kufuatilia fedha za mradi kila mara.


No comments:
Post a Comment