DKT. NATU APOKEA TUZO ZA MASHINDANO ZA UWASILISHAJI BORA WA HESABU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 10, 2025

DKT. NATU APOKEA TUZO ZA MASHINDANO ZA UWASILISHAJI BORA WA HESABU


Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Katikati), akipokea tuzo ya Wizara ya Fedha (Fungu 50), kutoka kwa PAT CPA. Nuru Mbekenga Abdallahmed (wa kwanza kushoto), baada ya Wizara ya Fedha kutangazwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya Uwasilishaji Bora wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2024, yaliyofanyika tarehe 4 Desemba 2025 jijini Dar es Salaam, ambapo ushindi huo unaifanya Wizara ya Fedha kuwa mshindi wa mara ya tano mfululizo katika nafasi mbalimbali tangu kuanza kushiriki kikamilifu mashindano hayo mwaka 2020. Wengine katika picha ni Manaibu Katibu Wakuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa kwanza kushoto) na Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia)

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Katikati), akipokea tuzo ya Wizara ya Fedha (Fungu 6), kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali Msaidizi, Mhandisi. Kenneth Nindie (wa pili kulia), baada ya Wizara ya Fedha kutangazwa mshindi wa tatu katika kipengele cha Idara za Serikali Zinazojitegemea (Independent Government Department) katika, mashindano ya Uwasilishaji Bora wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2024, yaliyofanyika tarehe 4 Desemba 2025 jijini Dar es Salaam, Wengine katika picha ni Manaibu Katibu Wakuu Wizara ya Fedha, Bw. Elijah Mwandumbya (wa kwanza kushoto) na Bi. Amina Khamis Shaaban (wa pili kulia)


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)











No comments:

Post a Comment