UFANISI KATIKA UHUDUMIAJI MELI BANDARI YA TANGA WAONGEZEKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, December 10, 2025

UFANISI KATIKA UHUDUMIAJI MELI BANDARI YA TANGA WAONGEZEKA




Na Oscar Assenga, TANGA

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA) umesema kwamba maboresho makubwa yaliyofanywa katika Bandari ya Tanga umepelekea wastani wa kuhudumia meli moja kwa siku tatu kutoka siku saba za awali kutokana na kuongezeka kwa ufanisi mkubwa.

Hayo yalisemwa na Mwakilishi wa Meneja wa Bandari ya Tanga Peter Milanzi wakati wa upokeaji aina mpya ya mzigo wa Lami kupitia Kampuni ya Wakala wa Usafirishaji ya Amura unaosafirishwa kwenda nchi jirani ya Malawi ambao wameamua kutumia Bandari hiyo kutokana na ufanisi wake

Alisema kwamba kutokana na ufanisi huo umepelekea kuvutia wateja wengi kuitumia Bandari hiyo kupitisha shehena mbalimbali za mizigo ikiwemo magari na mizigo mbalimbali ambazo zinakwenda nchi mbalimbali.

“Bandari ya Tanga tumeendelea kufanya vizuri kutokana na maboresho yaliyofanywa na Serikali kupitia Rais Dkt Samia Suluhu na hivyo kuvutia wateja wengi na leo tunapokea aina mpya ya mzigo wa Lami kwa wenzao wa Kampuni ya Amoue wameamua kuitumia Bandari ya Tanga kutokana na ufanisi ambao wanao kwa majaribio wameamua kupitisha makontena sita na kila moja lina mapipa 110 inaenda nchi ya Malawi”Alisema

Alisema kwamba hiyo ni ishara kubwa ya kuaminiwa na wafanyabiashara na watu mbalimbali hivyo wanawaambia wateja waendele kuitumia Bandari hiyo kutokana na wao wanaendelea kuwahudumia kwa ufanisi na kutoa huduma bora kama wenzao Amura.

“Bandari ya Tanga ni salama na itaendelea kuwa samana na kutoa huduma ya ushushaji wa mizigo na kwa wale waliokwama kwenye Bandari nyengine njooni Tanga mtahudumiwa kwa ufanisi mkubwa na kwa muda mfupi”Alisema Milanzi.

Hata hivyo alisema kwamba kuanzia mwezi Julai mwaka huu wa Fedha 2025/2026 walipangiwa kuhudumia Tani milioni 1.6 ,sasa wastani wa kuhudumia tani laki 137,000 lakini tokea mwezi Julai mwaka huu wamekuwa wakivuka malengo walianza na tani laki 152,000 na baadae wakapanda tani 157,000 na mwezi Septemba –Octoba wamefikisha tani 200,000 kila mwezi.


Alieleza kwamba wanaona malengo ambao wamewekewa watayafikia hayo yote yamekua kutokana na ufanisi wao kwenye kazi na hivyo wateja wameongezeka hatua inayoonyesha watavuta malengo waliopangiwa kutokana na m.

Awali akizungumza mara baada ya mara baada ya kushushwa kwa Shehena hiyo ya Lami –Mwakilishi wa Kampuni ya Amura ya Dar ,Zakaria Mohamed Nanimuka alisema kwamba kutokana na ufanisi wa Bandari ya Tanga wanategemea kuingiza kontena nyengine 20 zitazohudumiwa kwenye Bandari hiyo.

“Sisi kama Kampuni Amura tumefurahishwa na ufanisi wa Bandari ya Tanga na hakuna malalamiko wala changamoto zozote zile tunashukuru Serikali kwa kuwekeza hapa na sasa sisi wasafirishaji tutaendelea kuitumia katika kuingiza shehena mbalimbali”Alisema

Zakari alisema kwamba wamekuja Tanga kupokea shehena ya mzigo wa Lami kutoka Iran na kushukia Bandari ya Tanga kontena sita zenye tani 125 na kilo 430 ambapo kontena moja lina kuwa na pipa 110 kwa kontena

Alisema kwamba wanashukuru kwa namna walivyohudumiwa wamefanya kazi vizuri na wala hakukuwa na changamoto za aina yoyote ile mzigo wao umeweza kushughulikiwa wamepita scana kwa wakati hivyo wanamshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa maboresho makubwa yaliyosaidia kuongeza ufanisi.

No comments:

Post a Comment