MBUNGE JAFO AHIMIZA KASI YA UJENZI SHULE YA SEKONDARI DK.SELEMANI JAFO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, December 20, 2025

MBUNGE JAFO AHIMIZA KASI YA UJENZI SHULE YA SEKONDARI DK.SELEMANI JAFO



MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akikagua ujenzi wa mabweni mawili na madarasa katika Shule ya Sekondari Dkt.Selemani Jafo,wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe.


Na.Alex Sonna-Kisarawe


MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo, ameridhishwa na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa mabweni mawili na madarasa katika Shule ya Sekondari Dkt.Selemani Jafo, na kuhimiza Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha mradi huo unakamilika mapema ili ifikapo Januari 2026 shule hiyo iweze kupokea wanafunzi wa bweni.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe, Dkt. Jafo amesema ziara hiyo ni sehemu ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hususan katika sekta ya elimu.

“Tumeendelea na ziara yetu ya kuhakikisha tunasukuma utekelezaji wa ilani wilayani Kisarawe, na eneo kubwa tulilolipa kipaumbele ni uimarishaji wa sekta ya elimu. Hapa Shule ya Sekondari Selemani Jafo kuna kazi kubwa inaendelea, ikiwemo ujenzi wa mabweni mawili na madarasa ili kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu,” amesema.

Dkt. Jafo amepongeza usimamizi wa mradi huo, akieleza kuwa ujenzi umefikia zaidi ya asilimia 90, huku akielekeza Halmashauri kukamilisha haraka hatua zilizobaki ikiwemo uwekaji wa vigae.

“Ninapongeza sana usimamizi unaoendelea. Ujenzi umefikia zaidi ya asilimia 90, hivyo nimeelekeza Halmashauri ikamilishe kazi zilizobaki ili ifikapo Januari 2026 wanafunzi wakute miundombinu imekamilika,” ameongeza.

Aidha, amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuridhia kutoa fedha za ujenzi wa mabweni mawili na madarasa katika shule hiyo, hatua aliyosema inaonesha dhamira ya Serikali katika kuboresha elimu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kisarawe, Khalfan Sika, amesema miradi hiyo ni kielelezo cha utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa vitend“Nimshukuru sana Rais Samia kwa mapenzi makubwa kwa wana Kisarawe, lakini pia nimpongeze Mbunge wetu kwa kazi kubwa anayoifanya. Nina imani ifikapo Januari watoto wetu watasoma katika mazingira bora zaidi. Tunamuombea Rais na Mbunge wetu waendelee kutuhudumia wana Kisarawe,” amesema Sika.



MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akikagua ujenzi wa mabweni mawili na madarasa katika Shule ya Sekondari Dkt.Selemani Jafo,wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe.



MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa mabweni mawili na madarasa katika Shule ya Sekondari Dkt.Selemani Jafo,wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe.



MBUNGE wa Jimbo la Kisarawe, Dkt. Selemani Jafo,akizungumza na wananchi mara baada ya kukagua ujenzi wa mabweni mawili na madarasa katika Shule ya Sekondari Dkt.Selemani Jafo,wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Kisarawe.

No comments:

Post a Comment