
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI), Dkt. Jafar Seif, amesema kwa sasa TAMISEMI imewekeza nguvu kwenye uboreshaji wa huduma kwa wateja katika vituo vyake vyote vya kutolea huduma za afya msingi ili kuhakikisha mpango wa huduma ya Bima ya Afya kwa wote unaendana na a wa huduma kwa wateja
Naibu Waziri, Dkt. Seif ameyasema hayo wakati wa kikao cha wataalum kutoka OWM-TAMISEMI, Wizara ya Afya na NHIF waliokutana Jijini Dar es Salaam leo Desemba 31, 2025, kupeana taarifa na kujengeana uelewa wa pamoja juu ya hatua zilizofikiwa katika maandalizi ya utekelezaji wa mpango wa Bima ya Afya kwa Wote.
Naibu Waziri Dkt. Seif amesema “TAMISEMI hatutalala, lazima tulifanikishe hili la kuboresha huduma za Afya kwa wateja wetu, tunataka lugha e staha na wahudumu wa Afya wawahudumie wagonjwa wetu kwa upendo ili tunapoanza matumizi ya bima ya afya kwa wote mapema 2026, basi Watanzania waione thamani ya bima hiyo kwa vitendo”.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya Dkt. Florence Samizi amesisitiza kuwepo kwa utaratibu maalum utakaowezesha kushughulikia kwa urahisi na haraka, changamoto zozote zitakazojitokeza pindi tu utaratibu wa kusajili wateja katika mpango huo utakapoanza.
Timu hiyo ya wataalam imetumia kikao hicho kupitia maboresho ya sheria, mifumo na miongozo mbalimbali itakayowezesha ufanisi katika utekelezaji wa mpango huo wa Bima ya Afya kwa Wote.
Utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote ni miongoni mwa ahadi za kipaumbele za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alizoahidi kuzitekeleza ndani ya siku 100 za kwanza za kipindi cha uongozi wake wa awamu ya pili.




No comments:
Post a Comment