
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeungana na Jamhuri ya Kenya kwenye sherehe za maadhimisho ya kumbukizi ya uhuru wa Taifa hilo (Jamhuri Day), zilizofanyika katika Uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.
Katika sherehe hizo Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu Mhe. William Lukuvi (Mb) akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tanzania na Kenya zina uhusiano wa kidugu na kihistoria ambao umedumu kwa muda mrefu na unaendelea kuimarika siku hadi siku. Nchi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana katika nyanja za diplomasia, uchumi, siasa, usalama, utamaduni na kijamii na pia katika ngazi za Kikanda na Kimataifa, hususan kupitia Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Mataifa (UN).






No comments:
Post a Comment