WAKAZI WA MKOA WA SINGIDA WANUFAIKA NA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA MOYO: 26 WAPEWA RUFAA KWENDA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, December 5, 2025

WAKAZI WA MKOA WA SINGIDA WANUFAIKA NA UCHUNGUZI NA MATIBABU YA MOYO: 26 WAPEWA RUFAA KWENDA HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA


Na. Jeremiah Mbwambo


Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa kushirikiana na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida wameendesha kambi ya siku tano iliyo hitimishwa leo.

Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Moyo na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo John Meda amesema mwitikio umekuwa mkubwa wa wagonjwa 

"Watu wameitikia kwa wingi na kufikia lengo la kuwahudumia maana lengo letu ilikuwa ni kuwahudumia wananchi mpaka kufikia leo tumeona wananchi 176 tunatoa shukrani kwa uongozi walivyo jipanga kushirikiana nasi"amesema Dkt. Meda 


Kwa upande wake Bi. Irene Tandu mzazi wa mtoto aliye pewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Benjamin Mkapa ameeleza ni shauku yake kufika Hospitalini hapo ili kuendelea na matibabu 

"Ninawashukuru madaktari wamemuangalia mtoto wangu na wameniambia anatundu kwenye moyo, wamenipa dawa na wameniambia niende Hospitali ya Benjamin Mkapa ili mtoto amalizie matibabu yake na apone kabisa, nitamleta mtoto wangu kama nilivyoelezwa ili apate matibabu yote"amesema Bi. Irene 

Hospitali ya Benjamin Mkapa imeendelea kuzijengea uwezo Hospitali za kanda ya kati katika kutoa matibabu ya ubingwa.

No comments:

Post a Comment