
Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi - Huduma za Mfuko Mkuu, Wizara ya Fedha Bw. Perfectus Killenza, akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi la kutoa vitambulisho vya kielektoniki kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina kutoka Wilaya ya Dodoma Mjini, linaloendelea katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Mtunza Kumbukumbu, Wizara ya Fedha, Bi Zita Nyera, akiwaongoza wastaafu wa Wilaya ya Dodoma Mjini wanaolipwa na Hazina, waliofika kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya kielektroniki, katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wastaafu wa Dodoma Mjini, wanaolipwa na Hazina, linaloendelea katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mhasibu Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bi. Adolfina Bwanga, Akimhudumia msataafu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wastaafu wa Dodoma Mjini, wanaolipwa na Hazina, linaloendelea katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Mhasibu Mwandamizi, Wizara ya Fedha, Bi. Adolfina Bwanga, na Mtunza Kumbukumbu Pensheni, Wizara ya Fedha, Bi. Farida Mlanda, wakiendelea na zoezi la kugawa vitambulisho kwa wastaafu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, wanaolipwa na Hazina, waliofika kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya kielektroniki, katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wastaafu wa Dodoma Mjini, wanaolipwa na Hazina, linaloendelea katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.

Afisa Kumbukumbu Wizara ya Fedha, Bw. Timotheo Zingu na Mhasibu Mwandamizi, Wizara ya Fedha Bi Nuru Kiterebu, wakiendelea na zoezi la kugawa vitambulisho kwa wastaafu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, wanaolipwa na Hazina, waliofika kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya kielektroniki, katika zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wastaafu wa Dodoma Mjini, wanaolipwa na Hazina, linaloendelea katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma)
Na. Saidina Msangi na Jordan Mbwambo, WF, Dodoma.
Wastaafu wanaolipwa na Serikali wapatao 609 katika Wilaya ya Dodoma Mjini, wamepatiwa vitambulisho vya kielektroniki katika zoezi la kugawa vitambulisho hivyo linalotekelezwa na Wizara ya Fedha ambapo inalenga kuwafikia wastaafu wapatao elfu 50 nchini.
Hayo yalibainishwa na Mhasibu Mkuu wa Serikali Msaidizi- Huduma za Mfuko Mkuu, Wizara ya Fedha Bw. Perfectus Killenza, alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya zoezi la kutoa vitambulisho vya kielektoniki kwa wastaafu kutoka Wilaya ya Dodoma Mjini, linaloendelea katika Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.
Bw. Killenza alisema kuwa vitambulisho vya kielektroniki ni salama, imara na vinaondoa changamoto zilizokuwepo awali za vitambulisho vya karatasi ambavyo vilikuwa vikiharibika kwa urahisi na kufanya taarifa zisomeke kwa shida.
“Vitambulisho hivi vipya vitarahisisha upatikanaji wa huduma kwa wastaafu wetu kwa kuwa taarifa zao zitasomeka kwa urahisi kwa njia ya kielektroniki, sambamba na kuongeza ulinzi na uhakika wa kumbukumbu zao,” alisema Bw. Killenza.
Bw. Killenza alieleza kuwa zoezi hilo limekuwa muhimu pia katika kuboresha taarifa za wastaafu waliofanikiwa kufika Ofisi za Hazina kuchukua vitambulisho vipya jambo linaloondoa changamoto ya taarifa za baadhi ya wastaafu kutokusomana vizuri.
Pia Bw. Killenza alisisitiza wastaafu wote wa Wilaya ya Dodoma Mjini wanaohudumiwa na Hazina kufika katika Ofisi za Wizara ya Fedha wakiwa na nyaraka zao muhimu ili kurahisisha zoezi la kuhakikiwa na kupatiwa vitambulisho vipya vya kielektroniki kwa muda uliotajwa.
Bw. Killenza aliongeza kuwa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kielektroniki kwa wastaafu wote wanaolipwa na Hazina litafanyika nchi nzima kuanzia mwezi January mwaka 2026 kwa ratiba itakayotolewa.
Aidha, Bw. Killenza aliwakumbusha wastaafu wote wanaohudumiwa na Hazina kuwa huduma zote hususan zinazohusiana na pensheni ni bure hakuna gharama yoyote na hivyo kuwataka kuwa waangalifu ili kuepukana na matapeli.
‘’Wastaafu wote wanaolipwa na Hazina ni muhimu kuepuka watu au makundi yanayodai kuwawezesha kupata huduma kwa malipo, kwa kuwa kufanya hivyo kunaweza kuwaweka kwenye mtego wa udanganyifu na kupoteza fedha zao,’’alisisitiza Bw. Kilenza.
Kwa upande wao Wastaafu wanaolipwa na Hazina Bw. Selemani Ramadhani na Bi. Severina Kivangala ambao wamefanikiwa kupata vitambulisho vipya vya kielektroniki, wameishukuru Serikali kwa kufanikisha zoezi hilo na kuomba elimu iendelee kutolewa ili kuwawezesha wastaafu au warithi wao kupata mafao yao.
Wizara ya Fedha, inaendelea na zoezi la kugawa vitambulisho kwa wastaafu wanaolipwa na Hazina, katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, Jijini Dodoma, kwa muda wa siku kumi na nne (14) kuanzia tarehe 15 Desemba 2025 hadi tarehe 30 Desemba 2025.

No comments:
Post a Comment