
Na Sixmund Begashe, Mikumi
Hamasa ya watanzania kufanya utalii wa ndani iliyofanywa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji katika ziara mbalimbali alizozifanya kwenye taasisi za uhifadhi imezaa matunda kwa mamia ya watalii kujitokeza katika Hifadhi ya Mikumi kufanya utalii.
Akiwa katika zoezi la kuongonza mamia ya watalii waliojitokeza kwenye hifadhi hiyo, Dkt. Kijaji amesema, hayo ni matokeo chanya ya Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kuonesha njia kuhamasisha utalii kitaifa na kimataifa kupitia Filamu ya The Royal Tour
Amewapongeza wananchi wote waliojitokeza kwa wingi katika kufanya utalii kwenye vivutio vilivyopo nchini, huku akiwahakikishia kuwa Wizara anayoiongoza itawahudumia vyema watalii wote wanaoendelea kumiminika kwenye hifadhi za Taifa kujionea matunda adhimu ya uhifadhi wa maliasili zao.
Akiwa ambeambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Nkoba Mabula, Dkt. Kijaji ameendeleao kutoa wito kwa watanzania wote kuendelea kujitokeza kwa wingi kufanya utalii wa ndani, kwa kuwa nisehemu ya burudani na mafunzo pia.
Naye Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Agastin Masesa amepongeza jitihara za uongozi wa Wizara kwa hamasa kubwa waliyoitoa jambo linalipelekea kupokea wageni wengi kipindi hiki cha sikuku za mwisho wa mwaka.
Naye mtalii wa ndani kutoka Bereko Kondoa, Bi. Amina Iddi Mnyoti, amesema, utalii waliofunya umempa elimu kubwa zaidi ya matarajio yake kwa kuwa alitegemea kuburudika zaidi lakini amepata kujua tabia tofauti za wanyama na mimea.
Baada ya zoezi la kuongonza watalii, Mhe. Waziri Kijaji, atawaongoza watalii wote watakao lala Hifadhi ya Taifa Mikumi, kuupokea kuuwaga mwaka 2025 na kuupokea mwaka 2026 kwa sharma sharma maalum zilizoandaliwa na uongozi wa Hifadhi hiyo.


No comments:
Post a Comment