
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mheshimiwa Dkt Rhimo Nyansaho (Mb), Tarehe 30 Desemba, 2025 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania, Balozi Chen Mingjian katika ofisi ndogo za Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, jijini Dar-es-salaaam.
Balozi Chen Mingjian alimtembelea Waziri wa Ulinzi na JKT kwa ajili ya kujitambulisha na kufanya mazungumzo ya maeneo ya ushirikiano kati ya China na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga. Balozi Chen Mingjian alimshukuru Waziri wa Ulinzi na JKT kwa kukutana naye na akampongeza Waziri Nyansaho kwa kuteuliwa kwake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt Samia Suluhu Hassan, kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. akaishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha mahusiano imara ya kihistoria na muda mrefu kati ya Tanzania na China, alimueleza Waziri wa Ulinzi na JKT utayari wa Taifa la China kuendelea kushirikiana na Tanzania na katika masuala mbalimbali yanayohusiana ya Ulinzi na nchi kwa ujumla.
Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, alimshukuru Balozi kwa kufika Wizara y Balozi Chen Mingjian a Ulinzi na JKT kujitambulisha na kufanya naye mazungumzo yenye lengo la kuendeleza uhusiano wa kindugu na muda mrefu baina ya Tanzania na China, Waziri wa Ulinzi, Dkt Nyansaho alimuhakikishia Balozi Chen Mingjian kuwa Wizara ya Ulinzi na JKT ya Tanzania itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano uliopo wa nchi hizo mbili katika Diplomasia ya Kijeshi.
Mheshimiwa Dkt Rhimo Nyansaho, pia akamueleza Balozi wa China nchini kuwa Tanzania hususani Wizara ya Ulinzi inajivunia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu kati ya Tanzania na China katika masuala ya Biashara, Ulinzi na Utalii na miradi mbalimbali ya Maendeleo inayofanywa na serikali ya China nchini Tanzania.
Aidha Waziri Nyansaho akaipongeza Serikali ya China kupitia Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kupitia wizara ya Ulinzi na JKT katika maeneo ya Mafunzo, mazoezi ya pamoja na Huduma za Afya.








No comments:
Post a Comment