
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema December 07, 2025 usiku eneo la Tegeta Kinondoni lilimkamata aliyekuwa Waziri wa Uwekezaji na Mbunge wa Masasi, Geofrey Mwambe kwa tuhuma za jinai ambazo zinachunguzwa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro kwenye taarifa yake leo December 12, 2025 amesema "Hatua zaidi za kisheria zinakamilishwa"
Katika hatua nyingine Muliro amesema hali ya usalama jijini Dar es salaam ni nzuri na Wananchi wanaendelea na kazi halali mbalimbali.

No comments:
Post a Comment