ANGALIZO LA HALI MBAYA YA HEWA: UPEPO MKALI, MAWIMBI MAKUBWA NA MVUA KUBWA ZATARAJIWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 6, 2026

ANGALIZO LA HALI MBAYA YA HEWA: UPEPO MKALI, MAWIMBI MAKUBWA NA MVUA KUBWA ZATARAJIWA


⚠️ ANGALIZO LA HALI YA HEWA ⚠️


Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa:
Angalizo la upepo mkali unaofikia kasi ya kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa yanayofikia kimo cha mita 2 limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya ukanda wote wa pwani ya Bahari ya Hindi, yakijumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani (ikiwemo Visiwa vya Mafia), Lindi na Mtwara, pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Angalizo hili linaanza leo tarehe 06.01.2026 hadi 09.01.2026.

Mvua Kubwa:
Vilevile, angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe na Ruvuma kwa tarehe 08.01.2026.
Uwezekano wa Kutokea: Wastani

Kiwango cha Athari Zinazoweza Kutokea: Wastani


Wananchi wanaoishi katika maeneo husika wanashauriwa kuchukua tahadhari, kuzingatia maelekezo ya mamlaka husika na kuchukua hatua stahiki za kiusalama.



No comments:

Post a Comment