KASEKENYA ATOA MIEZI SABA KUKAMILIKA UJENZI WA OSBP MANYOVU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, January 17, 2026

KASEKENYA ATOA MIEZI SABA KUKAMILIKA UJENZI WA OSBP MANYOVU


Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amemtaka mkandarasi China Jiangxi International Economic and Technical Cooperation Co. Ltd anaejenga kituo cha forodha cha pamoja (OSBP) Manyovu/Mugina kuhakikisha kinakamilika ifikapo Julai mwaka huu.

Kituo hicho cha mfano cha forodha kinachojegwa Manyovu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma katika mpaka wa Tanzania na Burundi kinatarajiwa kuwaweka wadau wote wa huduma za mpakani na fedha katika eneo moja na hivyo kuchochea ukuaji wa biashara kati ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

"Ujenzi huu ukikamilika utachochea ongozeko la magari ya abiria na mizigo katika mpaka wa Manyovu na Mugina hivyo ni fursa kwa wananchi kuwekeza ili kunufaika na uwepo wake", amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Amesisitiza kuwa Serikali imedhamiria kuzijenga barabara zote kuu mkoani humo kwa kiwango cha lami katika kipindi kifupi ili kuboresha biashara kati ya Tanzania, Burundi na DRC hususan eneo la Kivu.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Massala Ngayalina ameishukuru Serikali kwa kuwekeza zaidi ya shilingi bilioni 47 kwenye ujenzi huo na kuahidi kuusimamia na kuulinda ili ulete ustawi kwa wananchì na taifa kwa ujumla.

Meneja wa Wakala wa Barabara TANROADS Mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amesema kituo hicho cha mfano pamoja na barabara unganishi ya juu zitajengwa kwa kizingatia thamani ya fedha na kukamilika kwa wakati.

Ujenzi wa OSBP ya Manyovu ni mkakati wa Serikali wa kuufungua mkoa wa Kigoma kwa kuuunganisha na nchi za Burundi na DRC kwa njia fupi na hivyo kukuza biashara na ujirani mwema baina ya mataifa hayo.

No comments:

Post a Comment