Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya e-GA mara baada ya uzinduzi rasmi wa bodi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa e-GA Mtumba - Dodoma.
Na: Mwandishi Wetu, Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete amezindua bodi ya ushauri ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) na kuitaka ihakikishe inaisimamia Mamlaka hiyo vyema na kutoa ushirikiano kwa menejimenti katika utatuzi wa changamoto zinazokwamisha utekelezaji wa majukumu yake.
Mhe. Kikwete ametoa wito huo leo Januari 27,2026.alipokuwa akizindua Bodi ya Ushauri ya e-GA katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo iliyopo Mtumba - Jijini Dodoma.
Mhe. Kikwete amempongeza Dkt. Mussa Kissaka kwa kuteuliwa na Rais kwa mara ya pili kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Serikali Mtandao na kumhakikishia ushirikiano wa dhati ili kutimiza malengo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya ujenzi wa Serikali Mtadao yenye tija.
“Ninafahamu Mamlaka imekuwa ikipata changamoto katika utekelezaji wa majukumu yake hasa pale taasisi zinaposhindwa kutekeleza sheria, kanuni, viwango na miongozo ya serikali mtandao, hivyo wekeni mikakati bora ya kudhibiti jambo hilo” alisisitiza Mhe. Kikwete.
Aidha, aliongeza kuwa moja ya mambo ambayo watumishi wa umma bado wanakiuka kwa makusudi au kwa kutofahamu ni suala la kutumia anuani za baruapepe ambazo sio za Serikali katika kutuma au kupokea taarifa za kiofisi jambo ambalo linasababisha kuvuja kwa siri za Serikali.
Pia, alisisitiza kuwa kila Wizara, Idara zinazojitegemea, Mamlaka za Serikali za Mitaa zinatakiwa kutumia anuani za baruapepe za Kiserikali zilizo kwenye utaratibu wa .go.tz, .gov, au .org katika kutuma au kupokea taarifa za kiofisi kwa njia ya baruapepe vinginevyo Sheria ichukue mkondo wake.
Vile vile, Mhe. Kikwete ametumia fursa hiyo kumtakia kila la kheri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku hii ya kuzaliwa kwake. Aidha, amemuombea dua kwa Mwenyezi Mungu ili amjalie Rais kheri, afya njema na umri mrefu ili aone wananchi wanavyonufaika na yale aliyoyaanzisha na kuyatekeleza kwa manufaa ya taifa.
Mhe. Kikwete amepanda mti wa muembe ikiwa ni ishara ya kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa. Mti huo umepandwa katika eneo la Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mtumba- Dodoma, tarehe 27 Januari, 2026.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akipanda mti wa muembe ikiwa ni ishara ya kumpongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika siku yake ya kuzaliwa. Mti huo umepandwa katika eneo la Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) Mtumba- Dodoma,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akifurahia jambo wakati akizindua Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) katika ukumbi wa mikutano wa e-GA Mtumba - Jijini Dodoma
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya e-GA mara baada ya uzinduzi rasmi wa bodi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa e-GA Mtumba - Dodoma

No comments:
Post a Comment