
NA. MWANDISHI WETU KILOSA
Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa leo Tarehe 2, Januari 2026 imekabidhi vifaa mbalimbali vya misaada ya kibinadamu kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa kwa Ajili ya waathirika wa Mafuriko Katika Kata ya Tindiga Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.
Makabidhiano ya vifaa hivyo yamefanyika Katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na yameongozwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. James Kilabuko, Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Brig. Jen. Hosea Ndagala na kapokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya.
Vifaa hivyo vilivyokabidhiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa ni Magodoro 90, Vyandarua 90, Mablanketi 90, Mahema 5 pamoja na Ndoo 90. Pia Ofisi ya Waziri Mkuu imetoa Unga Tani 7.2, Maharage Tani 2.1, Mafuta ya Kupikia Lita 360, Chumvi Kilo 300 na Sukari Kilo 600.



No comments:
Post a Comment