TUNA DENI LA KUSIMAMIA MIRADI NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI ILI KULETA MAENDELEO YA KWELI–MHE. SALOME - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, January 8, 2026

TUNA DENI LA KUSIMAMIA MIRADI NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI ILI KULETA MAENDELEO YA KWELI–MHE. SALOME


Na Mwandishi Wetu, SHINYANGA


Naibu Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Salome Makamba, amesema viongozi wana deni kubwa la kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo sambamba na kusikiliza pamoja na kutatua kero za wananchi ili kufanikisha maendeleo ya kweli.

Mheshimiwa Salome ameyasema hayo leo tarehe 8 Januari, 2026, mkoani Shinyanga wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya nishati inayotekelezwa mkoani humo.

Amesema wananchi wana imani kubwa na Serikali yao, hivyo ni wajibu wa viongozi kuhakikisha changamoto zinazojitokeza zinatatuliwa kwa wakati.

Ameongeza kuwa katika siku 100 za Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan Wizara ya Nishati imejipanga kuhakikisha umeme unawashwa kwenye miradi ya vitongoji mkoani Shinyanga ili kuwawezesha wananchi kunufaika na huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Salome ametembelea Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, ambapo alikutana na Katibu wa CCM Mkoa huo pamoja na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC) sambamba na Sekretarieti ya Mkoa ambapo amesema kumekuwa na ushirikiano mzuri kati ya Chama na Serikali katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake, Bi. Odilia Abraham Batimayo alisifu utendaji wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na TANESCO kwa kushughulikia kero na changamoto za wananchi kwa wakati, hatua inayochangia kujenga imani kwa wananchi kwa Serikali yao.

Mheshimiwa Salome yuko mkoani Shinyanga kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati, ikiwemo mradi wa umeme wa jua wa Kishapu pamoja na miradi ya umeme wa vitongoji katika vijiji mbalimbali vya mkoa huo.

No comments:

Post a Comment