WAZIRI KIKWETE AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NA MAMA ANNA MKAPA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, January 6, 2026

WAZIRI KIKWETE AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NA MAMA ANNA MKAPA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Mama Maria Nyerere (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Maria Nyerere (kulia), mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipomtembelea nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akifurahia jambo na Mama Anna Mkapa (kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa wakati alipomtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026.

Mama Anna Mkapa (wa kwanza kulia), mke wa Hayati Benjamin William Mkapa akimsindikiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (katikati) wakati Waziri huyo akiondoka baada ya kumtembelea nyumbani kwake Upanga Jijini Dar es Salaam kumjulia hali ikiwa ni utekelezaji wa majukumu yake leo tarehe 06 Januari, 2026. Wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Bw. Juma Mkomi.


Na. Veronica Mwafisi-Dar es salaam


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amewatembelea na kuwajulia hali Mama Maria Nyerere, mke wa Hayati Baba wa Taifa na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam na Mama Anna Mkapa, mke wa Hayati Benjamin William Mkapa nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam leo Januari 06,2026.

Mhe. Kikwete amesema, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anathamini sana mchango wa Viongozi Wakuu wa Kitaifa waliomtangulia na ataendelea kusimamia na kutunza familia hizo kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizowekwa.

Aidha, Mhe. Ridhiwani amesema, kuwatembelea na kuwajulia hali wake hao wa Viongozi Wastaafu ni moja ya majukumu yake ambayo anayatekeleza kwa lengo la kuwajulia hali, kusikiliza changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi kwa mujibu wa Katiba na Sheria zilizowekwa.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. Juma Mkomi amesema ofisi hiyo itafanyia kazi maoni na ushauri uliotolewa na wajane hao.

Aidha, Mama Maria Nyerere amemshukuru Mhe. Kikwete kwa kupata nafasi ya kumtembelea na kumjulia hali na amempongeza Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuijali familia yake wakati wote pasipo kuchoka.


Naye, Mama Anna Mkapa ameishukuru ofisi hiyo kwa kufuatilia kwa karibu masuala yanayowahusu na kuyatafutia ufumbuzi.

No comments:

Post a Comment