WAZIRI KIKWETE AWATEMBELEA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA WASTAAFU - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, January 9, 2026

WAZIRI KIKWETE AWATEMBELEA VIONGOZI WAKUU WA KITAIFA WASTAAFU


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimsikiliza Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein (kulia) wakati akizungumza nae alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Kibele, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini, Zanzibar tarehe 08 Januari, 2026

Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Mbweni, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini, Zanzibar tarehe 08 Januari, 2026.

Mama Sitti Mwinyi, mke wa Hayati Ali Hassan Mwinyi (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) alipomtembelea nyumbani kwake Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini, Zanzibar kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein (wa kwanza kulia) akisisitiza jambo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kulia) wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini, Zanzibar kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) baada ya kuzungumza nae nyumbani kwake Mbweni, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini, Zanzibar tarehe 08 Januari, 2026.

Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati la Viongozi wa Kitaifa Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo wakati Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani) alipomtembelea Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (hayupo pichani). Wengine ni wake wa Dkt. Bilal

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein (katikati) baada ya kuzungumza nae nyumbani kwake Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini, Zanzibar alipomtembelea kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Utawala na Dawati la Viongozi wa Kitaifa Wastaafu, Bi. Nyasinde Mukono.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal (watatu kutoka kulia). Wengine ni Wakurugenzi na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (kulia) akifurahia jambo na Mama Sitti Mwinyi, mke wa Hayati Ali Hassan Mwinyi (kushoto) baada ya kuzungumza nae alipomtembelea nyumbani kwake Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini, Zanzibar kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein (watatu kutoka kulia). Wengine ni Wakurugenzi na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mama Sitti Mwinyi (wa tatu kutoka kushoto), mke wa Hayati Ali Hassan Mwinyi wakati Waziri huyo alipomtembelea nyumbani kwake Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini, Zanzibar kumjulia hali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake. Wengine ni Wakurugenzi na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais-UTUMISHI.


Na. Veronica Mwafisi-Zanzibar


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amefikisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu ambaye ameahidi kuendelea kuwatunza Viongozi na Wenza wao kwa kuzingatia Katiba, Sheria na Kanuni zilizopo.

Salamu hizo zimefikishwa Januari 8, 2026 kwa nyakati tofauti alipomtembelea Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein nyumbani kwake Kibele Mkoa wa Kusini Unguja, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal nyumbani kwake Mbweni, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini na Mwenza wa Hayati Ali Hassan Mwinyi-Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwake Nyamanzi, Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini.

Mhe. Kikwete amesema, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ina jukumu la kutunza Viongozi Wakuu Wastaafu Kitaifa na Wenza wao, hivyo yuko tayari kuendelea kutekeleza jukumu hilo alilopewa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohammed Shein amemshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia kwa salaamu na kumpongeza Mhe. Kikwete kwa kupanga ziara ya kuwatembelea Viongozi Wakuu wa Kitaifa Wastaafu. Ziara hiyo inawapa faraja, heshima na inaonesha thamani ya mchango wao kwa taifa.

Aidha, Dkt. Shein ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa watumishi wa umma kufanya kazi kwa kupendana, ushirikiano na kuzingatia mipaka ya kazi zao kwa kuwa watumishi hao wanamsaidia Rais ambaye anawajibika kwa wananchi.

Naye, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal ameishukuru Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora kwa kuwajali na kuwahudumia vyema kwa mujibu wa taratibu


Kwa upande wake, Mama Sitti Mwinyi amemshukuru Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wenza wa Viongozi Wastaafu na ameomba moyo huo uendelee.

No comments:

Post a Comment