CCM SHINYANGA WAMPONGEZA SALOME MAKAMBA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 20, 2026

CCM SHINYANGA WAMPONGEZA SALOME MAKAMBA


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amempongeza Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba, kwa kutopandisha mabega kulingana na nafasi yake, na kuhudhuria kikao cha Baraza cha Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoani humo, licha ya kuwa na vikao vingi lakini ametanguliza chama kwanza.

Mabala ametoa pongezi hizo leo Februari 20, 2026, wakati akifungua kikao cha baraza cha UWT CCM mkoani humo.

Amesema, amefarijika kumuona Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba kwenye kikao hicho, pamoja na Mjumbe wa Mkutano wa SADC Mwanahamisi Munkunda, kwa kutanguliza Chama kwanza licha ya kuwa na vikao vingi, na kusema kwamba huo ndiyo uzalendo.

“Nakupongeza Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba kwa kuhuhuria kikao hiki cha baraza la UWT pamoja na mwenzako Mjumbe wa SADC Mwanahamisi, kutokana na nafasi zenu mgeweza kupandisha mabega na kutohudhuria kabisa na kutoa hudhuru kuwa mnavikao vingi, lakini kwa uzalendo wenu mmetanguliza chama kwanza,” amesema Mabala.


“Najua Salome una mkutano mwingine na ulipaswa kuwapo huko, lakini ukasema uhudhurie kwanza kwenye kikao hiki cha UWT hapa Shinyanga, nafasi yako uliyonayo upo kwa ajili ya kumsaidia Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na wanawake wa Shinyanga hongera sana kwa kuaminiwa na Rais na kuonyesha uzalendo,” ameongeza.

Aidha, amemmwagia pia sifa Salome Makamba, kwamba yeye siyo mtu wa maneno maneno wala kuwa na makundi, bali ni mtu wa kuchapa kazi na kutekeleza maagizo ambayo hupewa na kumsihi aendelee hivyo hivyo kukitumikia Chama na Taifa kwa ujumla kwa kuwaletea maendeleo wananchi kupitia Sekta ya Nishati.

Katika hatua nyingine Mabala amewaomba UWT Mkoani humo waendelee kuwa na umoja, mshikamano na upendo na kujiepusha na migogoro ili kuendeleza Jumuiya yao ipate kusongambele, na kuimarika zaidi.

Naye Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba, akizungumza kwenye kikao hicho, amesema amefarijika kuhudhuria kikao hicho, huku akiwashukuru UWT kwa kumpigia kura nyingi za ushindi Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025, pamoja na kumshukuru Rais kwa kumuamini na kumpatia dhamana ya kuwa Naibu Waziri wa Nishati, kwamba ataitendea haki nafasi hiyo kwa kuchapa kazi, na hatowaangusha wanawake wa Shinyanga.

“kwa mara ya kwanza UWT Mkoa wa Shinyanga imetoa Naibu Waziri wa Nishati kupitia Vitimaalum, hii dhamana ambayo nimepewa na Rais ni kubwa sana, sito waangusha wanawake wa Shinyanga nitachapa kazi kwa bidii zote kumsaidia Rais,” amesema Makamba.

No comments:

Post a Comment