POLISI WAFANYA UCHUNGUZI TUKIO LA MTU MMOJA KUFARIKI DUNIA. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, February 20, 2026

POLISI WAFANYA UCHUNGUZI TUKIO LA MTU MMOJA KUFARIKI DUNIA.



Jeshi la Polisi mkoani Arusha,  limesema linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio la mtu mmoja aitwaye Abdilah Musa maarufu kwa jina la Banjo ambaye alifariki dunia huko katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma.

Akitoa taarifa hiyo leo, Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo, amesema kuwa Jeshi hilo lilipokea taarifa kuhusiana na kupotea kwa mtu huyo Februari 13, 2026 ambaye inaelezwa alipotoea kuanzia Februari 12, 2026.

Kamanda Masejo amebainisha kuwa wakati wakiendelea na uchunguzi, februari 19, 2026 walipokea taarifa ya mtu huyo kuwa amefariki dunia huko mkoani Dodoma.

Aidha, amebainisha kuwa  pamoja na taarifa ambazo wameshazikusanya na wanazoendelea kuzikusanya, ametoa wito kwa mtu yoyote mwenye taarifa ambazo zinaweza kusaidia kufanikisha uchunguzi huu, asisite kuzitoa kwani watazipokea na kuzifanyia kazi kwa haraka

No comments:

Post a Comment