
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiagana na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake, Bw. Nathan Belete, baada ya kikao chao kilichofanyika katika ofisi za Benki hiyo, pembezoni mwa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF (2026 IMF/WBG Spring Meetings) inayoendelea jijini Washington DC, ambacho kilijadili miradi ya kipaumbele ya Serikali katika sekta mbalimbali itakayofadhiliwa na Benki hiyo kupitia Mzunguko wa 21 wa IDA (IDA-21 Cycle).

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (Katikati), Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayemaliza muda wake, Bw. Nathan Belete (Kulia), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Dkt. Tausi Kida, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika katika ofisi za Benki hiyo, pembezoni mwa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF (2026 IMF/WBG Spring Meetings) inayoendelea jijini Washington DC, ambacho kilijadili miradi ya kipaumbele ya Serikali katika sekta mbalimbali itakayofadhiliwa na Benki hiyo kupitia Mzunguko wa 21 wa IDA (IDA-21 Cycle).
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C, Marekani)

No comments:
Post a Comment