SERIKALI YATOA WITO KWA SEKTA BINAFSI KUSHIRIKI MIRADI YA MAENDELEO. - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 14, 2026

SERIKALI YATOA WITO KWA SEKTA BINAFSI KUSHIRIKI MIRADI YA MAENDELEO.


Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akizungumza wakati wa kikao na viongozi na wafanyakazi kutoka viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za vifungashio, madaftari na karatasi, walipomtembelea ofisini kwake, Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (kushoto), akikagua moja ya bidhaa ya kifungashio inayozalishwa na kiwanda cha vifungashio, baada ya viongozi na baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho pamoja na viwanda vidogo vingine walipomtembelea Mhe. Munde ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.

Kiongozi kutoka kiwanda cha vifungashio, Bw. Osman Haruni, ambaye pia aliongoza Ujumbe kutoka viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo karatasi, madaftari na vifungashio, akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), na Ujumbe huo kilichofanyika Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (kushoto), akiaga na na Kiongozi kutoka kiwanda cha vifungashio, Bw. Osman Haruni, ambaye pia aliongoza Ujumbe kutoka viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo karatasi, madaftari na vifungashio, baada ya kikao kilichofanyika ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.

Afisa Usimamizi wa Fedha, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Bw. Moses John (kushoto), akiwa na Katibu wa Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), Bw. Yambi Kinyaki, wakifuatilia kikao cha Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na viongozi na baadhi ya wafanyakazi wa baadhi ya viwanda vidogo walipomtembelea Mhe. Munde ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiongoza kikao chake na viongozi na wafanyakazi kutoka viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za vifungashio, madaftari na karatasi, walipomtembelea ofisini kwake, Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.

Ujumbe kutoka baadhi ya viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za vifungashio, madaftari na karatasi, ukiongozwa na Bw. Osman Haruni, kutoka kiwanda cha vifungashio (kulia), ukimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), wakati wa kikao na viongozi na wafanyakazi wa viwanda hivyo walipomtembelea ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (katikati), akiwa katika picha ya pamoja baadhi ya watumishi wa Wizara ya Fedha pamoja na baadhi ya viongozi na wafanyakazi kutoka viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za vifungashio, madaftari na karatasi, wakiongozwa na Bw. Osman Haruni, kutoka kiwanda cha vifungashio (wanne kulia), walipomtembelea ofisini kwake, Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF-Dodoma)


Na. Asia Singano na Jordan Mbwambo, WF – Dodoma.


Serikali imeendelea kuisihi sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi mbalimbali kwa kushirikiana na sekta ya umma kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, afya na miundombinu ili kuisaidia Serikali kufikia malengo yaliyowekwa katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), Ofisini kwake Wizara ya Fedha, Treasury Square jijini Dodoma, alipokutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi na wafanyakazi kutoka viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za vifungashio, madaftari na karatasi, walipomtembelea ofisini kwake.

Alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi katika kuhakikisha kuwa uchumi wa nchi unaendelea kukua na kuimarisha maisha ya Watanzania kama ilivyoelekezwa katika mpango wa maendeleo wa Taifa.

“Katika Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, tunalenga uchumi wa trilioni moja, ninyi ni wadau wakuu wa maendeleo ya nchi hii na tunataka ushiriki wenu uwe ni mkubwa kuliko upande wa Serikali kwa maana ya sekta ya umma’’ alisema Mhe. Mhandisi Munde.

Aliiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuendelea kudhibiti uingizwaji wa bidhaa kinyume na utaratibu ili kuongeza mauzo ya bidhaa zinazozalishwa hapa nchini ili kuongeza mapato ya nchi na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Munde aliwasisitiza wazalishaji wa bidhaa mbalimbali nchini kuendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuongeza ushindani katika soko la ndani na Kimataifa jambo litakalosaidia kuongeza mauzo.

Kwa upande wake kiongozi wa Ujumbe huo kutoka kiwanda cha vifungashio, Bw. Osman Haruni, ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono na kuweka mazingira rafiki ya biashara jambo linalowahamasisha wamiliki wa viwanda hivyo kuendelea na uzalishaji wa bidhaa hizo.


“Tuinashukuru Serikali inaendelea kutuunga mkono, tunaomba iendelee kutuwekea mazingira rahisi ya utekelezaji wa kazi zetu ili tuendelee kuzalisha bidhaa hizo kwa ubora zaidi” alisema Bw. Haruni.

No comments:

Post a Comment