MKENDA AKUTANA NA MABALOZI WATEULE, ELIMU YAWEKWA KIPAUMBELE CHA KIMATAIFA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 14, 2026

MKENDA AKUTANA NA MABALOZI WATEULE, ELIMU YAWEKWA KIPAUMBELE CHA KIMATAIFA


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda leo Aprili 14, 2026 jijini Dodoma amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wateule watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali walizopangiwa.

Katika kikao hicho wamekubalina kuwa elimu, sayansi na teknolojia zitakuwa moja ya agenda za kufanyia kazi ikiwemo suala la umataifishaji elimu.

Mabalozi wateule wameipongeza Wizara kwa mageuzi makubwa ya elimu yanayoendelea kutekelezwa na kuahidi kuichukua agenda ya elimu kuwa ya kimkakati kwa maendeleo ya taifa.

Mabalozi hao ni watakaoiwakilisha Tanzania Saudi Arabia, Zambia, Muscat
Comoros, Korea Kusini, Sweden na Umoja wa Mataifa, New York wakiongozwa na Mhe. Balozi Mhandisi Zena Said

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Katibu Mkuu, Manaibu Katibu Wakuu na baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Wizara hiyo.









No comments:

Post a Comment