KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MFUMO WA UAGIZAJI MAFUTA NCHINI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, February 19, 2026

KAMATI YA BUNGE YARIDHISHWA NA MFUMO WA UAGIZAJI MAFUTA NCHINI


Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati, Mhe. Subira Mgalu, ameipongeza Serikali kwa kazi kubwa inayofanyika katika kuhakikisha mafuta nchini yanapatikana kwa wakati, kwa uwazi na kwa kuzingatia viwango stahiki.

Ametoa pongezi hizo tarehe 19 Februari 2026 wakati wa ziara ya kamati hiyo katika miundombinu ya upokeaji mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam pamoja na matanki ya kuhifadhia mafuta katika eneo la Kigamboni na Kurasini,.

Ameeleza kuwa mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja unawezesha Serikali kufahamu kwa usahihi kiwango cha mafuta kilichoagizwa, kinachoingizwa nchini na kinachowafikia waagizaji, sambamba na kuhakikisha takwimu zinaendana na kuwa na uwazi katika ukusanyaji wa tozo mbalimbali.

“Tumeshuhudia kazi kubwa iliyofanywa na Serikali pamoja na watendaji wa PBPA katika kuhakikisha mafuta yanapatikana kwa wakati na kwa uwazi. Huu ni mfumo unaotoa uhakika na unaolinda maslahi ya taifa, tunawapongeza sana kwa usimamizi huu,” amesema Mhe. Mgalu

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amebainisha kuwa, mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja umeongeza ufanisi na kuaminika hata katika nchi jirani.
“Huu nii mfumo unaoaminika hata na nchi jirani ambazo zimekuwa zikitumia bandari zetu kupitisha mafuta kutokana na uwazi na usimamizi madhubuti uliopo." Amesema
Ameongeza kuwa kwa sasa Serikali ina akiba ya kutosha ya mafuta, huku ikipokea zaidi ya aina tatu za mafuta ikiwemo petroli, dizeli, mafuta ya mitambo na mafuta ya ndege.
.
Naye Mtendaji Mkuu wa PBPA, Bw. Erasto Simon amesema kuwa mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja umewezesha Serikali kufanikisha ukusanyaji wa mapato kwa asilimia 100 ya kodi stahiki kutokana na mpangilio wa zabuni za uagizaji wa mafuta kufanyika miezi miwili kabla hivyo Mamlaka ya Mapato sasa inaweza kukadiria mapato yatakayopatikana hata miezi miwili kabla ya kipindi husika.

Bw. Erasto amesema lengo kuu la uwekezaji huo, ni kuhakikisha nchi inakuwa na akiba ya kutosha ya mafuta wakati wote ili kuepusha changamoto ya upungufu, pamoja na kulinda ubora wa mafuta yanayoingia sokoni.

No comments:

Post a Comment