MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE KITAIFA HAYAFUNGAMANI NA ITIKADI YOYOTE: DKT. GWAJIMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, February 17, 2026

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE KITAIFA HAYAFUNGAMANI NA ITIKADI YOYOTE: DKT. GWAJIMA




Na Mwandishi Wetu- Dodoma 


Katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya wanawake Machi 8,2026 Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima amesema maadhimisho hayo hayafungamani na itikadi yoyote bali ni kwa ajili ya wanawake wote kwa ushirikiano na wanaume wote ambao ni wadau wakubwa kwenye kufanikisha maazimio ya Ulingo wa Beijing, 1995.


Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo leo Februari 17,2026 Jijini Dodoma wakati akizungumza na vyombo vya habari kuelekea siku hiyo ambayo kwa mwaka huu wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yatafanyika kila mkoa ngazi zote kuanzia kijiji/mtaa, kata, halmashauri, wilaya hadi mikoa.


"Sare ya maadhimisho itakuwa Vazi la Batiki kwa kadri Mkoa utakavyochagua lengo likiwa ni kuendelea kuwainua wajasiriamali wa ndani hivyo, wazalishaji wa batiki wa ndani katika kila mkoa watambuliwe na kutumika kutengeneza batiki za kutosheleza mahitaji kwenye Mkoa husika,"amesema. 


Katika hatua nyingine Waziri huyo amesema, Wizara itaungana na mkoa wa Geita kuadhimisha na tarehe 30 Machi, 2026, itatoa tathmini ya hali ya ushiriki wa kila mkoa kwenye kuadhimisha. 


"Lengo la kuungana na Mkoa wa Geita ni mkoa wenye changamoto ya ukatili wa kijinsi na tunataka tukawaelimishe wananchi wa kule kutokana na kukumbwa na kadhia hiyo lakini pia ukiangalia takwimu za ukatili zipo juu hivyo tunapenda kuona zikipungua, "amesema. 

Amesema Maadhimisho hayo yatafanyika kuanzia tarehe 01 hadi 08 Machi, 2026 ambapo watafanya mikutano katika kila Kijiji/Mtaa ya Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi huku mikutano hiyo ikitumika kuhamasisha uundaji wa vikundi vya wanawake na maendeleo ya ujasiariamali.


"Maadhimisho kwa mwaka 2026 nchini Tanzania yataongozwa na kaulimbiu isemayo Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050 na kwamba, inalenga kujenga uelewa wa kuwekeza kwenye Maendeleo Jumuishi ikiwemo, kutambua Haki za Wanawake na Wasichana  na kuhakikisha zinafanyiwa kazi kwa vitendo na kuleta mabadiliko ya kweli,"amesema. 

No comments:

Post a Comment