Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi leo Februari 26, 2026 jijini Dodoma amekutana na kufanya kikao na Wadau wakuu wa kukabiliana na migogoro ya wanyama wakali na waharibifu (HWC) ili kuja na mikakati madhubuti zaidi ambapo amewataka wadau hao kuunganisha nguvu zaidi.
Ameyasema hayo katika kikao kilichowashirikisha wataalamu wa serikali na wale wa asasi za kiraia na sekta binafsi kikilenga kuweka mikakati madhubuti kwa kushirikiana na wadau hao ili kupunguza au kudhibiti kabisa migogoro ya wanyama wakali nchini.
Amewaeleza wadau hao kuunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo tayari imefanya juhudi mbalimbali za kudhibiti wanyama wakali kwa kuwekeza katika teknolojia ya ndege nyuki(drones), ujenzi wa vizimba vya kuzuia mamba, matumizi ya mabomu baridi na kutoa elimu kwa umma.





No comments:
Post a Comment