Na Mwandishi Wetu-Dodoma
Taasisi ya Lugha ya Kichina (Confucius Institute) ya Chuo Kikuu cha Dodoma kwa kushirikiana na Shule ya Sekondari Dodoma, imeadhimisha Sherehe za Mwaka Mpya wa Kichina 2026 kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa kitamaduni na kielimu kati ya Tanzania na China.
Maadhimisho hayo yaliyofanyika Jijini Dodoma Februari 18,2026 yaliwakutanisha wanafunzi, walimu na wageni mbalimbali kushuhudia maonesho ya utamaduni wa Kichina, zikiwemo ngoma za jadi, muziki na mafunzo ya lugha.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Naibu Makamu Mkuu wa Chuo - Mipango, Fedha na Utawala akimwakilisha Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM Prof. Jefta Sunzu alisema ushirikishwaji wa wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kwenye sherehe kama hizo kunachochea hamasa ya wanafunzi kuendelea kujifunza lugha hiyo kwa ufasaha zaidi na kugundua fursa zilizopo.
"Wanafunzi hawa wanakuja kuwaona Watanzania wachache ambao tayari wanaweza kuzungumza kichina, hivyo wanapojitokeza kwenye hizi sherehe ni hamasa kwao na kwa wale ambao bado wako ngazi ya chini watapata hamasa ya kusoma masomo ya Kichina, "alisema.
Aidha, alitoa rai kwa wanafunzi kuchangamkia fursa ya kusoma lugha hiyo kwani watawekeza na kujiandaa na fursa mbalimbali zinazojitokeza na kuwa tayari kuzichukua.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Lugha ya Kichina Bi. Amber alisisitiza umuhimu wa kujifunza lugha na tamaduni kama daraja la kuimarisha ushirikiano wa kimataifa.
Alibainisha kuwa sherehe hizo zililenga kuwapa wanafunzi nafasi ya kujifunza kwa vitendo kuhusu mila, desturi na falsafa ya Wachina, huku wakijenga heshima kwa utofauti wa tamaduni duniani.
Kwa upande wake Shule ya Sekondari Dodoma kupitia kwa mwalimu wao wa Kichina Khalid Mohamed alieleza kuwa ushirikiano huo umefungua fursa mpya kwa wanafunzi, ikiwemo kujifunza lugha ya Kichina na kushiriki katika programu za kubadilishana uzoefu wa kielimu.
Sherehe hizo zilidhihirisha kuwa elimu haiishii darasani pekee, bali pia hujengwa kupitia mwingiliano wa tamaduni, Mwaka Mpya wa Kichina 2026 ni sherehe ya mshikamano, maarifa na matumaini mapya kwa wanafunzi wa Kitanzania.

No comments:
Post a Comment