UJENZI WA KIWANDA CHA KUCHAKATA PAMBA SIMCU (2018) LTD WAFIKA ASILIMIA 75 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Saturday, February 21, 2026

UJENZI WA KIWANDA CHA KUCHAKATA PAMBA SIMCU (2018) LTD WAFIKA ASILIMIA 75


Naibu Mrajis - Uhamasishaji, Consolata Kiluma, amekipongeza chama kikuu cha Ushirika SIMCU (2018) LTD, kwa usimamizi wa ujenzi wa ujenzi na ukarabati wa kiwanda cha kuchakata pamba kilichopo wilayani Maswa mkoa wa Simiyu ambacho kinatarajiwa kuanza kazi musimu huu wa 2026/2027.

Ametoa pongezi hizo leo Februari 21, 2026 alipofanya ziara katika chama hicho kwa lengo kukagua na kuona hatua zilizofikiwa za ujenzi kuelekea uzinduzi wake.

Aidha amewataka viongozi wa SIMCU (2018) LTD, kuendelea kufufua viwanda vingine vinavyomilikiwa na chama ambavyo havifafanyi kazi kwa sasa ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirika wa viwanda ili kuongeza thamani ya mazao ya wakulima.

Naye, Mwenyekiti wa SIMCU (2018) LTD, Ramadhani Matani, amesema juhudi mbalimbali zinaendelea kuhakikisha kiwanda kinaanza kufanya kazi haraka iwezekanavyo ambapo mpaka sasa wamefikia zaidi ya asilimia 75 ya ujenzi wa kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment