
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, leo Machi 4, 2026, ametembelea Ofisi za Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) jijini Dar es Salaam na kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mwinjuma amesisitiza umuhimu wa Bodi kusimamia sheria kikamilifu bila kupepesa, kuhakikisha kanuni zinaimarishwa, kufuatilia na kudhibiti wanaofanya kazi za habari bila ithibati ili kulinda hadhi ya taaluma.
Mhe. Mwinjuma amepongeza juhudi za Bodi, huku akisisitiza kuwa utekelezaji wa sheria haupaswi kulegalega ili kuimarisha weledi, uwajibikaji na imani ya umma kwa vyombo vya habari nchini.

Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, pamoja na kuelezea utekelezaji wa majukumu, amefafanua mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuzinduliwa kwa bodi ikiwemo uanzishaji wa mifumo ya usajili wa Waandishi, utoaji wa Ithibati na Vitambulisho vya Uandishi (Press Cards), utoaji wa elimu kwa umma, usimamizi wa maadili ya taaluma na uandaaji wa nyaraka zote muhimu za uanzishwaji wa Taasisi chini ya Msajili wa Hazina.



No comments:
Post a Comment