MHE. SALOME AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI TANESCO MKOA WA KIGOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Friday, March 6, 2026

MHE. SALOME AZUNGUMZA NA WAFANYAKAZI TANESCO MKOA WA KIGOMA


Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Wafanyakazi wa TANESCO Mkoa wa Kigoma ambapo pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya amewataka kuongeza nguvu katika utekelezaji wa mipango ya Serikali ya kuboresha huduma za nishati.

Mhe. Salome ametoa pongezi hizo tarehe 6 Machi 2026 wilayani Kigoma, Mkoa wa Kigoma akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya nishati.

" Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wanatambua mchango wenu katka sekta ya umeme, hata hivyo mnapaswa kuongeza kasi ya kuunganishia umeme wateja ili tuweze kufikia pia lengo la mpango wa misheni 300 linalotutaka kuunganiaha wateja wapya milioni 8 ifikapo 2030." Amesema Mhe.Salome

Aidha, amesema katika kuongeza kasi ya usambazaji wa umeme, TANESCO Kigoma itapokea gari la kunyanyulia mizigo (crane) litakalosaidia katika utekelezaji wa kazi za kiufundi na kuimarisha huduma za umeme.

Vilevile, Mhe. Salome ameitaka TANESCO kuhakikisha kuwa wananchi wanaoishi katika maeneo ambayo ni lazima kuvuka kwa kutumia boti iwanafikiwa kwa kutenga bajeti ya kununua boti maalum kwa ajili ya kazi za kufuatilia miradi na usambazaji umeme.

Pia amewahimiza watendaji TANESCO kuwa wabunifu na kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa, ikiwa ni pamoja na kupeleka elimu hiyo katika maeneo ya masoko, stendi na maeneo mengine ya mikusanyiko ya watu.

Awali, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Hassan Nganjau alisema mkoa huo sasa unapata umeme wa uhakika kupitia gridi ya Taifa ambapo mahitaji ya juu ya umeme ni megawati 27.

Alieleza kuwa, awali mkoa huo ulikuwa ukizalisha umeme kwa kutumia majenereta, hali iliyosababisha kuwepo kwa mgao wa umeme katika baadhi ya nyakati. Hata hivyo, baada ya kuunganishwa na gridi ya Taifa, upatikanaji wa umeme umeimarika na sasa umeme ni wa uhakika.

Alisema uwepo wa umeme wa gridi umepelekea Serikali kuokoa takribani shilingi bilioni 58 kwa mwaka zilizokuwa zikitumika kwa ununuzi wa mafuta na matengenezo ya vipuri vya majenereta.

Vilevile alisema kutokana na upatikanaji huo wa umeme wa uhakika, TANESCO imeweza kuunganisha wateja wengi wakiwemo wa viwanda na pia kuvutia wawekezaji katika sekta mbalimbali.

"Katika mwaka huu wa fedha, TANESCO Kigoma tumeweza kuunganisha wateja 23,224 na kuvuka lengo la kuunganisha wateja 16,000." Alisema Mhandisi Nganjau

Kwa upande wa vijiji alisema vijiji vyote 306 vya Mkoa wa Kigoma tayari vina umeme. Aidha, kati ya vitongoji 1,858, vitongoji 1,436 tayari vina umeme huku wakandarasi wakiendelea na kazi ya kusambaza umeme katika vitongoji 316. Lengo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 vitongoji vyote vinakuwa vimefikiwa na umeme.

Katika ziara yake mkoani Kigoma, Naibu Waziri wa Nishati ameambatana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ( Umeme na Nishati Jadidifu), Mhandisi Edson Ngabo.

No comments:

Post a Comment