NAIBU WAZIRI MAGHEMBE AANZA ZIARA YA KIKAZI NCHINI INDIA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, March 4, 2026

NAIBU WAZIRI MAGHEMBE AANZA ZIARA YA KIKAZI NCHINI INDIA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe.Dkt. Ngwaru Maghembe ameanza ziara ya kikazi nchini India ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje katika Jukwaa la Raisina 2026 utakaofanyika jijini New Delhi kuanzia tarehe 5 hadi 7 Machi, 2026

Akiwa nchini humo, Mhe. Maghembe ambaye anamwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo kwenye ziara hiyo, pia atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt. Subrahmanyam Jaishankar, Wawakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini humo pamoja na kuzungumza na Diaspora.

Mhe. Maghembe amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega ambaye pamoja na Maafisa wa Wizara na Ubalozi, wametoa taarifa ya maandalizi ya ziara hiyo katika kikao kilichofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi, New Delhi - India.









No comments:

Post a Comment