RAIS DKT.MWINYI:MASHINDANO YA QURAAN YANAIWEKA TANZANIA KWENYE RAMANI YA KIMATAIFA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, March 1, 2026

RAIS DKT.MWINYI:MASHINDANO YA QURAAN YANAIWEKA TANZANIA KWENYE RAMANI YA KIMATAIFA


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Mashindano Makubwa ya Kimataifa ya Quraan Tukufu kwa mabara yote duniani yameendelea kuwa chachu ya kuimarisha mapenzi ya Quraan, kujenga maadili kwa vijana na kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa kwa heshima ya kuandaa mashindano kwa kiwango cha juu.

Amesema hayo leo tarehe 01 Machi, 2026 katika mashindano yaliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, yaliyoandaliwa na Al Hikma Foundation, yakihusisha washiriki kutoka mabara mbalimbali duniani.

Rais Dkt. Mwinyi amesisitiza kuwa mashindano hayo si jukwaa la ushindani pekee, bali ni sehemu ya kuimarisha heshima ya taifa, kuendeleza misingi ya Tajweed na Hifdh kwa viwango vya kimataifa, pamoja na kulea kizazi chenye maadili na imani thabiti.

Washindi wa Mashindano ya Kimataifa ya Quraan Tukufu 2026:
1.     Abdulrahman Yasin, Uganda – 97% – USD 12,000 2.     Mohamed Mustafa, Canada – 96.5% – USD 8,000 3.     Shueyb Mohamed, Sweden – 96.2% – USD 5,000 4.     Bilal Ahmad, Réunion – 95% – USD 4,000 5.     Bilal Hassen, New Zealand – 94.5% – USD 3,000

Rais Dkt. Mwinyi amewapongeza washiriki wote kwa ustadi wao mkubwa, akibainisha kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya juhudi binafsi, malezi bora ya walimu na msaada wa familia.

 Amehimiza jamii kuendelea kuisoma, kuielewa na kuifanyia kazi Quraan kama nuru na mwongozo wa maisha ya kila siku ili kujenga taifa lenye mshikamano na maadili mema.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi wa Dini, Serikali, Mabalozi, Wanazuoni wa Kiislamu na Maelfu ya Wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio hilo la kihistoria lenye hadhi ya kimataifa. 

No comments:

Post a Comment