Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dodoma imeonesha mafanikio ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya miundombinu wakati wa maadhimisho ya siku 100 za Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza Machi 5, 2026 katika viwanja vya Nyerere Square, Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Colman Gaston Ramadhani, amesema miradi yenye thamani ya mabilioni ya shilingi inaendelea kutekelezwa na tayari inaleta maendeleo kwa wananchi.
Ametaja baadhi ya miradi hiyo kuwa ni Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 410, Barabara ya Mzunguko wa Dodoma yenye zaidi ya bilioni 230 pamoja na Barabara ya Ntyuka iliyogharimu zaidi ya bilioni 39.
Pia amesema TANROADS imetekeleza kwa mafanikio miradi ya dharura (CERC) yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5 ambayo imekamilika kwa asilimia 100.
Katika maadhimisho hayo, TANROADS imeweka banda maalum katika viwanja vya Nyerere Square kwa ajili ya kutoa taarifa za miradi na kusikiliza maoni ya wananchi. Hadi sasa zaidi ya wananchi 80 wamefika kutoa maoni na kuuliza maswali kuhusu miundombinu ya barabara.
TANROADS imewahimiza wakazi wa Dodoma kutembelea banda hilo ili kujionea miradi inayotekelezwa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.












No comments:
Post a Comment