Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Wilfred Mwakalosi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la EWURA wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya bunge jijini Dodoma. ....
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), leo 21 Aprili 2026, imetumia fursa ya Wiki ya Nishati kuwahamasisha waheshimiwa wabunge kuwekeza katika ujenzi wa vituo vya mafuta maeneo ya vijijini pamoja na vituo vya CNG ili kuendelea kusogeza huduma kwa wananchi.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, Bw. Wilfred Mwakalosi, alisema kuwa EWURA inatumia maonesho hayo kutoa elimu kuhusu namna inavyohakikisha upatikanaji wa huduma za nishati na maji kwa wakati na kwa gharama nafuu.
Amebainisha kuwa wabunge ni wawakilishi wa wananchi, hivyo kuwajengea uelewa kuhusu udhibiti, fursa za uwekezaji na utaratibu wa kupokea na kushughulikia migogoro na malalamiko kutawawezesha kuwasilisha taarifa sahihi kwa wananchi kuhusu juhudi za Serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za umeme, mafuta na gesi asilia.
Akizungumza katika maonesho hayo, Ofisa Mwandamizi wa Kitengo cha Mafuta, Mhandisi. Ibrahim Kajugusi, amesema elimu inayotolewa pia inalenga kuwafahamisha wananchi jinsi EWURA inavyosimamia upatikanaji wa huduma za mafuta nchini kwa kuzingatia ubora uliopitishwa na gharama sahihi.
Aidha, amewahamasisha wananchi kuchangamkia fursa za uwekezaji katika sekta hiyo, hususan ujenzi wa vituo vya mafuta vya gharama nafuu vijijini na mijini pamoja vituo vya kujazia gesi asilia kwenye magari (CNG).
Kwa upande wake, Mchumi wa EWURA Bi. Achilana Mtingele,amesema elimu inayotolewa imejikita katika kueleza namna EWURA inavyosimamia upangaji wa viwango vya bei za huduma za umeme, mafuta na gesi asilia. Aliongeza kuwa mamlaka hiyo huweka mizania kati ya maslahi ya watoa huduma na watumiaji, na kwamba wabunge waliopata elimu hiyo wataweza kuiwasilisha ipasavyo kwa wananchi katika maeneo yao.
Akizungumzia sekta ya gesi asilia, Mhandisi Mwandamizi wa Gesi Asilia, Mhandisi Evaline Rweikiza, amesema EWURA itaendelea kusimamia ubora wa miundombinu ya gesi asilia nchini na kuhamasisha matumizi yake, hususan katika magari.
Amebainisha kuwa hadi sasa vituo 18 vimepata leseni ya EWURA kutoa huduma ya gesi asilia, huku vituo sita vingine vikiwa katika hatua za mwisho za kupata leseni katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani. Aidha, mipango inaendelea kwa baadhi ya makampuni kusambaza gesi asilia iliyokandamizwa katika mikoa ya Morogoro na Dodoma.
Kwa upande wa sekta ya umeme, Mhandisi Mwandamizi wa Umeme, Lulu Chilumba, amewahamasisha wabunge na wadau wanaotembelea maonesho hayo kutumia mafundi umeme wenye leseni kutoka EWURA ili kuhakikisha usalama wa nyumba na mali zao. Alisema EWURA inaendelea kutoa leseni kwa mafundi umeme wenye sifa stahiki, ambapo zaidi ya leseni 1,000 zilitolewa katika mwaka wa fedha uliopita.
Naye Ofisa Rasilimali Watu Mkuu, Bi. Limi Kahabi, amesema EWURA ni mwajiri anayezingatia misingi ya usawa na haki katika mchakato wa ajira, akisisitiza kuwa taasisi hiyo huajiri kwa kuzingatia sifa, weledi na usawa kwa wote.

Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Wilfred Mwakalosi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la EWURA wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Wilfred Mwakalosi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la EWURA wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.

Kaimu Meneja wa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Wilfred Mwakalosi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la EWURA wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mchumi wa EWURA Bi. Achilana Mtingele,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la EWURA wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Ofisa Mkuu, Usimamizi wa Rasilimali Watu,Bi. Limi Kahabi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la EWURA wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mhandisi Mwandamizi wa Umeme, Lulu Chilumba,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la EWURA wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Ofisa Mwandamizi wa Kitengo cha Mafuta, Mhandisi. Ibrahim Kajugusi,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la EWURA wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.
Mhandisi Mwandamizi wa Gesi Asilia, Mhandisi Evaline Rweikiza,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye banda la EWURA wakati wa maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika viwanja vya bunge jijini Dodoma.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa katika picha ya pamoja siku ya pili ya Maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayofanyikia katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) wakiwa katika picha ya pamoja siku ya pili ya Maonesho ya Wiki ya Nishati 2026 yanayofanyikia katika Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma

No comments:
Post a Comment