SERIAKLI YAELEZA DHAMIRA YAKE KUWAWEZESHA VIJANA KIUCHUMI - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, April 20, 2026

SERIAKLI YAELEZA DHAMIRA YAKE KUWAWEZESHA VIJANA KIUCHUMI

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akizungumza katika Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza alipokuwa mgeni Rasmi katika mahafali hayo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), (kushoto), akiteta jambo na Meneja wa Shule ya Sekondari Thaqaafa, Bw. Idrisa Hayeshi, wakati wa Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya shule hiyo iliyopo wilayani Nyamagana jijini Mwanza alipokuwa mgeni Rasmi katika mahafali hay.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi, wakati wa Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza.

Wahitimu wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Thaqaafa, wakimsikiliza Mgeni Rasmi wa Mahafali ya 20 ya shule hiyo, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika shuleni hapo jijini Mwanza.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Thaqaafa, Bw. Jafar Kubelabo, akizungumza katika Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza
Picha za matukio mbalimbali wakati wa Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF - Dodoma)


Na Asia Singano na Josephine Majura, WF, Mwanza.


Serikali imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sera na mipango mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), katika Mahafali ya 20 ya Shule ya Sekondari ya Thaqaafa, wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.

Alieleza kuwa, Serikari inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kupitia Sera na mipango mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha kuwa vijana wanapata fursa za kuendeleza vipaji vyao na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa.

‘’Dunia ya sasa inahitaji vijana wanaoweza kutatua changamoto kwa ubunifu, hasa katika nyanja za uchumi, teknolojia na ujasiriamali ‘’ Alisema Mhe. Munde (Mb).

Amewaasa vijana kuendelea kuwa na nidhamu na uadilifu kwakuwa Taifa linahitaji vijana wenye misingi imara ya maadili, wanaoweza kusimamia rasilimali za nchi kwa uwajibikaji na weledi.

Kwa upande wake Meneja wa Shule ya Thaqaafa, Bw. Idrisa Hayeshi, amewasisitiza wazazi kuendelea kushirikiana na walimu na Uongozi wa shule kufuatilia maendeleo ya wanafunzi ili kujua mwenendo wa tabia ambazo zina athari katika masomo yao.

“Shule imejipanga kutoa elimu bora ikiwa na matokeo mazuri kwa kila mwaka, tunavyofanya mawasiliano na mzazi ni kwamba atoe ushirikiano ili mtoto apate kitu kinachostahili’’ alisema Bw. Hayeshi.

Shule ya Sekondari Thaqaafa imeadhimisha Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ambayo yalihudhuriwa na wahitimu (50).

No comments:

Post a Comment