TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU KUTOLEWA APRILI 13, 2026 DAR ES SALAAM - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, April 8, 2026

TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU KUTOLEWA APRILI 13, 2026 DAR ES SALAAM



Na Okuly Julius, OKULY BLOG , Dodoma


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inataraji kutoa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu Aprili 13, 2026 jijini Dar es Saalam, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, ambaye alikuwa nguli katika uandishi bunifu.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, amesema hayo leo Aprili 8,2026 jijini Dodoma, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya utoji tuzo hiyo hafla itakayofanyika wiki ijayo.

Prof. Mkenda, amesema lengo la tuzo hiyo ni kukuza vipaji vya uandishi bunifu kwa Watanzania, kukuza utamaduni wa kusoma vitabu, kulinda na kuhifadhi historia, utamaduni na tunu za taifa Tanzania.

Pia, kukuza sekta ya uchapishaji vitabu nchini Tanzania pamoja na kuongeza hifadhi ya vitabu katika maktaba na nje ya mipaka.

“Tunayofuraha kwa mara ingine kuwatangazia umma wa watanzania kuwa wakati umewadia wa kutoa tuzo za Tuzo Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu kwa mwaka 2026.

“Tuzo hii hutolewa kila ifikapo tarehe 13 ya mwezi Aprili ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambae pia alikuwa nguli katika uandishi bunifu, hivyo kutambua mchango wake katika kukuza lugha adhimu ya Kiswahili, kutunza utamaduni na tunu za Taifa letu,”amesema Prof. Mkenda

Amesema, katika kuendesha hafla hiyo kwa mukatadha wa dhamira yake, itatanguliwa na mjadala utakaohudhuria na waandishi bunifu maarufu nchini Tanzania pamoja na wageni mashuhuri wawili ambao ni Dk. Aida Mutenyo kutoka nchini Uganda na Ferdinand Ndahayo kutoka nchini Rwanda.

Kadhalika, alisema tangu kuanzishwa kwake wadau mbalimbali wamekuwa wakishiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini yaani Tanzania Bara na Zanzibar pamoja na nje ya nchi.

Hata hivyo, amesema, wadau hawa wanatoka katika kada na makundi mbalimbali kama vile, waandishi wa habari, wakulima, askari polisi, wafanyabiashara, wajasiriamali, walimu na wanafunzi.

Mwenyekiti wa Kamati kuu ya tuzo hizo Prof. Penina Mlama, alisema mchakato wa uendeshaji tuzo hiyo umejumuisha upokeaji na usomaji wa miswada 260 ulifanywa na jopo la majaji.

Prof. Mlama, amesema mchakato huo umefanyika kwa kipindi cha mwaka mzima, ambapo hivi sasa wanaelekea kilele cha utoaji tuzo yenyewe ambayo hafla ya utoaji itafanyika Aprili,13, 2026.







No comments:

Post a Comment