WANANCHI 2,682 KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTAMBO WA KUTIBU NA KUSAFISHA MAJI KAHAMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, April 21, 2026

WANANCHI 2,682 KUNUFAIKA NA MRADI WA UJENZI WA MTAMBO WA KUTIBU NA KUSAFISHA MAJI KAHAMA

Na Mwandishi Wetu- Dodoma 

Serikali imesema ujenzi wa mtambo wa kutibu na kusafisha maji (treatment plant) katika eneo la Buzwagi Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga umefikia wastani wa asimilia 78 za utekelezaji na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2026 huku wananchi wapatao 2,682 wa eneo la Lugela wakitarajiwa kunufaika na mradi huo. 

Hatua hiyo imebainishwa leo Aprili 21,2026 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew wakati akijibu swali la Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Benjamin Ngayiwa aliyehoji Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa chujio la maji la Buzwagi na tenki la maji la Shunu/Lugela ili kupunguza kero ya kukatika kwa maji Kahama.

Aidha, Mha. Mathew amema Serikali kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi inaendelea na mradi wa ujenzi wa mtambo wa kutibu na kusafisha maji (treatment plant) katika eneo la Buzwagi Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

"Utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 79 na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2026,"amesema. 

Vilevile amebainisha kuwa, Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji Lugela unaojumuisha ujenzi wa tanki la maji lenye ujazo wa lita 75,000 katika eneo la Lugela Kata ya Nyahanga wilayani humo. 

"Kazi zingine zinazotekelezwa ni pamoja na ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 9 ambapo umeanza kutoa huduma kwenye baadhi ya maeneo ya Lugela,"amebainisha.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment