
Kongamano la 5 la Wahasibu wa Afrika Mashariki(EACOA2026) linatarajia kuanzia Aprili 22 hadi 24 Jijini Bujumbura Nchini Burundi ambalo litakutanisha washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)
Aidha Kongamano hilo ambalo linatajwa kuwa miongoni mwa mikutano mikubwa na yenye ushawishi katika sekta ya fedha na uhasibu katika ukanda wa Afrika Mashariki, linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Burundi, Meja Jenerali, Evariste Ndayishimiye.
Kwamujibu wa taraifa iliyotolewa na waandaaji, zaidi ya washiriki 150 kutoka nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na wadau wa kimataifa, wataalamu wa fedha, viongozi wa serikali, mashirika ya kimataifa na sekta binafsi wanatarajiwa kushiriki katika kongamano hilo.
Miongoni mwa washiriki ni Yuvenali Shirima ambaye ni Mtaalamu na mbobezi wa masuala ya kibiashara,Kodi fedha na maendeleo ya kiuchumi amethibitishwa kuhudhuria kongamano hilo ambaye ataitangaza Tanzania Kimataifa kutokana na ushiriki wake
Ambapo mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa kisasa wa AGATEKA HALL uliopo ndani ya majengo ya Bunge la Burundi wenye hadhi ya juu unaokidhi viwango vya kimataifa na unaotumika kwa mikutano mikubwa ya kitaifa na kimataifa.
Kongamano la mwaka huu linaongozwa na kaulimbiu isemayo “Driving Sustainability through Innovation in the Accounting Profession”ambapo kaulimbiu hiyo inalenga kuonesha namna taaluma ya uhasibu inavyoweza kuwa chachu ya maendeleo endelevu kupitia matumizi ya teknolojia za kisasa,uwazi na uwajibikaji katika mifumo ya kifedha,pamoja na ubunifu katika usimamizi wa rasilimali za kiuchumi.
Katika dunia inayokabiliwa na changamoto za kiuchumi zinazotokana na migogoro ya kimataifa, mabadiliko ya teknolojia na ushindani wa kiuchumi, mkutano huu unatarajiwa kutoa majibu ya kitaaluma yatakayosaidia kuimarisha uchumi wa nchi za Afrika Mashariki.
Katika kongamano hilo, Yuvenali Shirima anatarajia kuchangia mambo mbalimbali ya kitaaluma ikiwemo
uwezeshaji wa vijana na wanawake katika sekta ya fedha na uhasibu,nafasi ya wataalamu wa fedha katika kukabiliana na changamoto za uchumi wa dunia,kuimarisha uwazi, uwajibikaji na uadilifu katika mifumo ya kifedha,matumizi ya teknolojia katika kuboresha ufanisi wa uhasibu na ukaguzi.
Ambapo ushiriki wake unatazamwa kama sehemu ya juhudi za kuendeleza ushirikiano wa kitaaluma kati ya Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki, pamoja na kuongeza mchango wa vijana katika majukwaa ya kimataifa.
Kongamano hilo ni tukio la kila baada ya miaka miwili likiwa jukwaa muhimu linalowakutanisha wataalamu wa uhasibu na wadau wa maendeleo ili kujadili mustakabali wa uchumi wa ukanda wa Afrika Mashariki,changamoto za uwazi na matumizi ya fedha za umma
ushirikiano wa kikanda katika sekta ya fedha,nafasi ya teknolojia katika kuboresha mifumo ya kifedha
Pia ushiriki wa Shirima katika kongamano hilo unaonyesha nafasi ya vijana wa Tanzania katika majukwaa ya kimataifa, ambapo wanapata fursa ya kubadilishana uzoefu na wataalamu wa kimataifa,kujifunza mbinu mpya za usimamizi wa fedha,ujenga mtandao wa kitaaluma ,kuchangia mawazo katika sera na mwelekeo wa uchumi wa kikanda.
Hatua hiyo pia inaonyesha umuhimu wa kuendelea kuwawezesha vijana kushiriki katika majukwaa ya kimataifa ili kuchochea maendeleo ya taifa.
Shirima ni Mkurugenzi Mkuu wa YURASHI KILIEDU CONSULTANCY, kampuni inayojihusisha na masuala ya ushauri wa kitaalamu katika sekta ya Kodi, Biashara, fedha na maendeleo ya kiuchumi pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Vijijini akijihusisha na uongozi wa vijana na maendeleo ya kijamii huku akiendelea kujenga mchango wake katika majukwaa ya kitaifa na kimataifa.

No comments:
Post a Comment