WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda, akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wanu Hafidh Ameir,akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Caroline Nombo,akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mapitio ya Sheria y Elimu Wakili Frida Mwera ,akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
Katibu wa Kamati ya Mapitio ya Sheria ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Wakili Innocent Mgeta ,akizungumza katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
SEHEMU ya wadau wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda,(hayupo pichani) katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
SEHEMU ya wadau wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof Adolf Mkenda,(hayupo pichani) katika kikao cha kuwasilisha kwa wadau taarifa ya awali ya kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, sura ya 353 kilichofanyika leo Mei 21,2026 jijini Dodoma.
Na Okuly Julius, OKULY BLOG , DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, ametoa wito kwa wadau wa elimu nchini kuongeza kasi ya utoaji wa maoni katika mchakato wa mapitio ya Sheria ya Elimu ili kuhakikisha sheria hiyo inaendana na mageuzi yanayoendelea kufanywa katika sekta ya elimu nchini.
Profesa Mkenda amesema hayo leo Mei 21, 2026 jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha wadau wa elimu kilicholenga kuwasilisha taarifa ya awali ya Kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu, Sura ya 353.
Amesema serikali imeendelea kufanya maboresho mbalimbali katika sekta ya elimu ikiwemo kuandaa sera mpya ya elimu ambayo tayari imezinduliwa, huku hatua inayofuata ikiwa ni kufanya maboresho ya sheria ili kuendana na mwelekeo mpya wa elimu ifikapo mwaka 2028.
“Tunakutana kwa ajili ya kupitia mapendekezo ya sheria ambayo tayari yamefanyiwa kazi. Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 imefanyiwa marekebisho kadhaa, lakini sasa tunakusanya maoni yatakayosaidia kuamua kama tuje na sheria mpya au tufanye maboresho zaidi,” amesema Profesa Mkenda.
Aidha amesema maoni yatakayokusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali yatawasilishwa katika Baraza la Mawaziri kwa hatua zaidi za maamuzi, huku akibainisha kuwa serikali inalenga kuhakikisha waraka huo unakamilika ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Profesa Mkenda pia amewashukuru wadau wa sekta ya elimu kwa ushiriki wao katika kutoa maoni na michango inayolenga kuboresha mfumo wa elimu nchini.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, amesema mchakato huo umechukua muda mrefu kwa lengo la kuhakikisha inapatikana sheria inayozingatia maoni ya wananchi wengi pamoja na wadau wa elimu.
Amesema Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 imeweza kudumu kwa muda mrefu hivyo ipo haja ya wadau kutoa maoni yatakayosaidia kupatikana sheria bora itakayodumu kizazi hadi kizazi huku maslahi ya taifa yakiwekwa mbele.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa amesema wizara imejipanga kuyachakata na kuyafanyia kazi maoni yote yatakayowasilishwa na wadau kwa maslahi mapana ya maendeleo ya sekta ya elimu nchini.
Hata hivyo, Profesa Nombo amewataka washiriki kuwa wazi katika kutoa maoni yao ili kusaidia kupatikana kwa sheria bora yenye manufaa kwa taifa.
Wadau mbalimbali wa elimu wanaamini kuwa mapitio ya sheria hiyo yatachangia kuboresha mfumo wa elimu nchini na kuendana na mahitaji ya sasa pamoja na dira ya maendeleo ya Taifa.

No comments:
Post a Comment