BENKI YA MAENDELEO AFRIKA (AFDB) KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII AFRIKA (ASSA) KUIMARISHA UCHUMI AFRIKA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, June 1, 2026

BENKI YA MAENDELEO AFRIKA (AFDB) KUSHIRIKIANA NA JUMUIYA YA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII AFRIKA (ASSA) KUIMARISHA UCHUMI AFRIKA




Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) na Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya nchi za Afrika (ASSA) imesaini mkataba wa ushirikiano kwa lengo la kuiwezesha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika nchi za Afrika kushiriki kwa ufanisi katika uwekezaji wa miradi ya kimkakati ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya kiuchumi na kijamii katika bara la Afrika itakayoimarisha ukuaji wa ukwasiu na uhimilivu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, kuboresha huduma na mafao kwa wanachama wake na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya bara la Afrika.

Makubaliano hayo yalifanyika katika kilele cha Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) yaliyofanyika tarehe 28 Mei, 2026 huko Brazzaville, Congo na kusainiwa na Bw. Meshach Bandawe, ambaye ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ya nchi za Afrika (ASSA) na Bw. Ahmed Attout, Mkurugenzi wa sekta ya fedha wa benki hiyo na kushuhudiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dr Sidi Ould Tah.
Ushirikiano huo pia utajikita katika kujenga uwezo wa kuendelea kuimarisha sekta ya Hifadhi ya Jamii Afrika ikiwa ni pamoja na msaada wa kiufundi ili kuwafikia watu wengi zaidi wanaopaswa kukingwa na sekta ya Hifadhi ya jamii na pamoja na kutumia rasilimali za ndani na mapato ya ndani katika nchi za Afrika katika uwekezaji wa miradi ya miundombinu inayolenga kuleta tija kwa Mifuko na manufaa kwa wanachama wake pamoja na kuchangia Maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi za Afrika ikiwemo kutengeneza ajira, kupunguza umaskini, kuimarisha pato la Taifa na ubora wa maisha ya watu wa Afrika.


Pamoja na kukabiliwa na nakisi katika tekelezaji wa miundombinu, Afrika bado inaendelea kuimarisha sekta mbalimbali za miundombinu ikiwemo usafirishaji kama vile barabara, reli, viwanja vya ndege na Bandari, Nishati, mawasiliano ya kidijitali, viwanda, kilimo nk zitakazowezesha kuwa na muunganiko wa kibiashara wa kikanda katika bara la Afrika kama ilivyoanishwa katika agenda ya Maendeleo ya kijamii ya Imoja wa Afrika (African Union Social Agenda 2026)


Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ilianzishwa nchini Rwanda na Makao Makuu yake kuwa Jijini Arusha Tanzania kwa lengo la kuiwezesha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika bara la Afrika kufanya kazi kwa pamoja, kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya Hifadhi ya Jamii kama vile kuongeza wigo wa wanachama, kuimarisha mifumo ya utendaji, kuimarisha sera na miongozo ya Hifadhi ya jamii, kuboresha mafao, masuala ya Uwekezaji na kuimarisha huduma kwa wanachama kwa kutumia mifumo ya teknolojia ya kisasa.




Hivi karibuni kamati ya utendaji ya Mawaziri wa sekta ya miundombinu na Nishati y Umoja wa Afrika (AU) ulipitisha azimio la kuendelea kuipa nguvu Jumuiya ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika ili kuimarisha shughuli zake.


No comments:

Post a Comment