WAITARA ATAKA WABADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA WANYONGWE - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Tuesday, June 2, 2026

WAITARA ATAKA WABADHIRIFU WA FEDHA ZA UMMA WANYONGWE



Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali kutafakari uwezekano wa kuweka adhabu ya kunyongwa kwa watu wanaobainika kufanya ubadhirifu wa fedha za umma.

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma Juni 2, 2026 wakati wa mjadala wa bajeti ya Wizara ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2026/27, Waitara alisema kuwa vitendo vya ubadhirifu wa fedha za umma vinawakosesha wananchi huduma muhimu, ikiwemo upatikanaji wa dawa hospitalini.

“Kunao wananchi katika majimbo yetu wanaokwenda hospitalini na kukosa dawa kutokana na ukosefu wa fedha, lakini wakati huo huo kuna watu wachache wanaotuhumiwa kutumia vibaya mamia ya mamilioni ya shilingi za umma. Serikali inapaswa kuchukua hatua kali zaidi dhidi ya wanaobadhirifu fedha za umma,” amesema Waitara.

Aliongeza kuwa nchi nyingine zimekuwa zikichukua hatua kali dhidi ya watuhumiwa wa rushwa na ufisadi, akitolea mfano wa China ambapo baadhi ya wahusika wa makosa makubwa ya rushwa wamewahi kukabiliwa na adhabu kali.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la matumizi ya fedha za umma tunapaswa kusimama imara. Tumeona katika baadhi ya nchi wahusika wa rushwa kubwa wakichukuliwa hatua kali sana. Hata hapa kwetu, wanaoiba fedha za wananchi wanapaswa kukabiliwa na adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine,” amesema.

No comments:

Post a Comment