WIZARA YA ELIMU YAWEKA MKAZO KATIKA TEHAMA, TAKWIMU NA DIRA 2050 - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Monday, July 13, 2026

WIZARA YA ELIMU YAWEKA MKAZO KATIKA TEHAMA, TAKWIMU NA DIRA 2050

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,akizungumza wakati akifungua kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo leo Julai 13,2026 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia,Prof. Daniel Mushi,akizungumza wakati wa kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo leo Julai 13,2026 jijini Dodoma.

Sehemu ya washiriki wakifuatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo,(hayupo pichani) wakati akifungua kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo leo Julai 13,2026 jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.

Na.Okuly Julius ,OKULY BLOG -DODOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, amezitaka taasisi zote za elimu nchini kuunganisha mifumo yao ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Elimu (ESMIS), akisema hatua hiyo ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa takwimu sahihi zitakazowezesha Serikali kufanya maamuzi yenye tija na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma.

Prof. Nombo alitoa maelekezo hayo leo Julai 13, 2026 jijini Dodoma alipokuwa akifungua kikao cha mwaka cha Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya wizara hiyo, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda.

Alisema hatua hiyo pia inatekeleza maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha mifumo yote ya Serikali inasomana na kubadilishana taarifa kwa ufanisi, jambo litakalorahisisha upangaji na utekelezaji wa mipango ya maendeleo.

Mbali na kuimarisha matumizi ya ESMIS, Prof. Nombo alitoa maagizo mengine yanayolenga kufanya mapitio ya mara kwa mara ya kozi na programu za elimu ili ziendane na mahitaji ya sasa ya jamii, uchumi na soko la ajira, pamoja na kuongeza ushiriki wa sekta binafsi katika uwekezaji wa elimu.

Aidha, alisema kikao hicho ni fursa ya kutathmini mafanikio yaliyofikiwa na kuweka mikakati ya kuhakikisha sekta ya elimu inatoa mchango mkubwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Daniel Mushi, aliwataka viongozi na watendaji wa sekta ya elimu kuendelea kueleza mafanikio yanayopatikana kupitia utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali za Serikali ili wananchi waendelee kutambua jitihada zinazofanyika kuboresha elimu nchini.

No comments:

Post a Comment