MHADHIRI UDOM AJITOSA UBUNGE CHAMWINO - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Wednesday, September 30, 2026

MHADHIRI UDOM AJITOSA UBUNGE CHAMWINO



NA FRED ALFRED , DODOMA


MHADHIRI wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk. Frank Menda, amejitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea Ubunge wa Jimbo la Chamwino, akisema dhamira yake ni kuwatumikia wananchi.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Dk. Menda amesema amejipima na kuona ana uwezo wa kuwa kiongozi na kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Chamwino.

“Nilitia nia na nikajipima nikaona naweza kabisa kuwa kiongozi kwa kuwatumikia wananchi wa Jimbo la Chamwino,” amesema.

“Kilichonisukuma ni kuwatumikia tu wananchi. Na kuwa kiongozi ni maisha ya binadamu kuwa kiongozi. Ameondoka huyu, anakuja kiongozi mwingine,” amesema.

Amesema hatua ya kuchukua fomu ni sehemu ya mchakato wa kuomba ridhaa ya CCM, huku akisisitiza kuwa dhamira yake ni kutumia nafasi hiyo iwapo atapewa ridhaa na wananchi kumchagua, kuwatumikia na kushughulikia masuala yanayowahusu.

No comments:

Post a Comment