.jpeg)
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imewataka Makarani Waongozaji Wapiga Kura katika kata ya Nonde iliyopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya Mkoani Mbeya kutekeleza majukumu yao kwa weledi.
Hayo yamebainishwa leo Oktoba 31, 2026 na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele wakati akizungumza na watendaji hao alipotembelea mafunzo yao ya siku moja ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata ya Nonde unaotarajiwa kufanyika tarehe 04 Novemba,2026.
Jaji Mwambegele amewasisitiza washiriki hao kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni ili kuufanya uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.
Awali kabla ya ufunguzi wa Mafunzo haya, washiriki hao waliapa kiapo cha kutunza siri na kile cha kujitoa uanachama wa chama cha siasa ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa haki na weledi.
Uchaguzi huo utafanyika ikiwa ni miongoni mwa kata kata 11 za Tanzania Bara ambazo ni Lugenge, Halmashauri ya Mji Njombe; Bargish, Halmashauri ya Mji Mbulu; Makole, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza; Mwera, Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Oldonyosambu, Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Nyingine ni Igalula iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui; Shelui, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba; Mvumi, Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa; Nyarero, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Ilolangulu, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe.
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

No comments:
Post a Comment