KILIMANJARO, HUDUMA YA MAJI KUZIDI KUIMARISHWA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Sunday, October 4, 2026

KILIMANJARO, HUDUMA YA MAJI KUZIDI KUIMARISHWA


Watendaji wa Sekta ya Maji mkoa wa kilimanjaro wametakiwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa majisafi pamoja na kuchukua tahadhari hasa katika maeneo yenye miundombinu dhaifu katika kukabiliana na mvua za El nino kama ilivyo tabiriwa na Mamlaka ya Hali ya hewa (TMA).

Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Kundo Andrew Mathew (Mb) ameyasema tarehe 4 Oktoba 2026 Moshi, Kilimanjaro katika kikao na watendaji wa Sekta ya Maji.

Amesema katika kuboreshaji huduma ya maji watendaji waendelee kufanyia kazi agizo la Rais Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan la ufungaji wa dira za malipo ya kabla.

Amesisitiza kasi ya ufungaji wa dira hizo kwa taasisi zote,sekta binafsi ikiwemo hoteli na viwanda iongezeke ili kuepukana na changamoto ya upotevu wa maji (NRW) na wizi ili huduma ya usambazaji maji iwafikie wateja wengi na kuchangia ongezeko la mapato.

Amesema maboresho hayo ni sehemu ya kuhakikisha wakazi wa Kilimanjaro wanaendelea kupata huduma ya majisafi na salama ya uhakika.






No comments:

Post a Comment