
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akieleza madhumuni ya ziara yake alipokutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Wilaya ya Ngorrongoro, ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile, katika Ofisi za Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha.

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile, akitoa taarifa ya Wilaya hiyo, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), Wilayani hapo inayolenga kujionea uhitaji wa Kituo cha kutoa huduma za Forodha.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akisani kitabu cha wageni alipowasili Wilaya ya Ngorongoro kwa ziara ya kikazi, kujionea uhitaji wa Kituo cha kutoa huduma za Forodha. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile.

Wajumbe wa Mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile (hawapo pichani), wakifuatilia Mkutano huo wakati wa Ziara ya Mhe. Munde Wilayani Ngorongoro Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiongoza kikao kati yake na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile, alipowasili kujionea uhitaji wa Kituo cha kutoa huduma za Forodha katika eneo la Loliondo na Sale, mkoani Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akikaribishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile, alipowasili kujionea uhitaji wa Kituo cha kutoa huduma za Forodha katika eneo la Loliondo na Sale, mkoani Arusha.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akikaribishwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Mhe. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile, alipowasili kujionea uhitaji wa Kituo cha kutoa huduma za Forodha katika eneo la Loliondo na Sale, mkoani Arusha.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiteta jambo na baadhi ya viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha, alipowasili kwa ziara ya kikazi, kujionea uhitaji wa Kituo cha kutoa huduma za Forodha katika eneo la Loliondo na Sale, Wilayani hapo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha)
Na Peter Haule, WF, Ngorongoro
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), amewasili Wilaya ya Ngorongoro, Mkoani Arusha, kwa ajili ya ziara ya kikazi yenye lengo la kujionea uhitaji wa kuanzishwa kwa Kituo cha Huduma za Forodha katika maeneo ya mpakani mwa Tarafa za Loliondo na Sale.
Mhe. Munde amepokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Luteni Kanali Robert Augustino Kakomangile, pamoja na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo.
Ziara hiyo inafanyika kufuatia ombi la Mbunge wa Ngorongoro, Mhe. Yannick Ndoinyo, ambaye aliomba aambatane na Naibu Waziri kutembelea maeneo ya mpakani ili kujionea hali halisi na mahitaji ya wananchi, hususan uhitaji wa Kituo cha Huduma za Forodha.
Baada ya kuwasili wilayani humo, Mhe. Munde alifanya mazungumzo na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali wa eneo hilo.
Katika mazungumzo yao, Mhe. Munde aliwapongeza viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma stahiki kwa wakati.
Alisema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na zinazokidhi mahitaji yao.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Mhe. Luteni Kanali Kakomangile, alimshukuru Mhe. Munde kwa kutembelea wilaya hiyo, akisema ziara hiyo ni sehemu ya kuimarisha ukaribu kati ya Serikali na wananchi.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri Mhe. Munde anatarajiwa kutembelea maeneo ya mpakani katika Kijiji cha Njoroi, Kata ya Ololosokwan, Tarafa ya Loliondo, pamoja na Kijiji cha Olmiti, Kata ya Enguserosambu, Tarafa ya Loliondo, Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.
Ziara hiyo inalenga pia kupata uelewa wa hali halisi ya maeneo hayo na mahitaji yaliyopo kuhusu huduma za Forodha.

No comments:
Post a Comment