MWINYI AKABIDHIWA OFISI YA CCM KIGOMA - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 1, 2026

MWINYI AKABIDHIWA OFISI YA CCM KIGOMA


Kaimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma, ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (MNEC), Ndugu Khalidi Mwinyi, leo Oktoba 1, 2026, amekabidhiwa rasmi Ofisi na aliyekuwa Katibu wa CCM Mkoa huo, Ndugu Pallangyo Christopher.

Makabidhiano hayo yamefanyika kufuatia mabadiliko ya makatibu wa CCM yaliyofanywa hivi karibuni, ambapo jumla ya Kaimu Makatibu wapya 32 waliteuliwa katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Ofisi, Mwinyi amesema amepata matumaini makubwa baada ya kuiona Sekretarieti ya CCM Mkoa wa Kigoma na kwamba anaamini uongozi huo utaendelea kujenga mafanikio yaliyopatikana.

“Nimeiona Sekretarieti ya CCM Mkoa na kupata matumaini ya hatua kubwa zaidi. Uongozi ni mwendelezo; tunaheshimu tulipokuta, tunaboresha tulipo na tunajenga tunakokwenda,” amesema Mwinyi.

Mwinyi amesisitiza umuhimu wa kuendeleza mazuri yaliyofanywa na uongozi uliopita, huku akieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa utekelezaji wa majukumu ya Chama kwa maslahi ya CCM na wananchi.







No comments:

Post a Comment