Meneja wa Mfuko wa PSSSF, Zanzibar, Bi. Mariam Salehe (kulia), akiungana na Wanachama wa Mfuko Visiwani Zanzibar kwenye Wiki ya Huduma kwa Wateja katika ofisi ya PSSSF, mjini Unguja.
Afisa Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa PSSSF, Bi. Mwajuma Msina (kushoto) akimuhudumia mwanachama wa Mfuko Bi. Ndeashi Ndossa, wakati wa Kampeni inayoendelea ya Mlango kwa Mlango kwa waajiri, Mkoani Kilimanjaro kwenye Wiki ya Hduuma kwa Wateja.

Kwenye Wiki ya Huduma kwa Wateja inayoelekea ukingoni Mfuko wa PSSSF Mkoani Ruvuma umeungana na Wanachama na Wastaafu katika kukata keki ikiwa ni ishara ya kuonyesha ushirikiano kati yao.
Afisa wa Mfuko wa PSSSF Mkoani Geita akimuhudumia Mwanachama wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Meneja wa Mfuko wa PSSSF Kanda Ya Magharibi, Bw. Eliad Mndeme (kulia) akimuhakiki Mstaafu Bw. Doto Elias aliyefika kwenye Ofisi za PSSSF Tabora kwenye Wiki ya Huduma kwa Wateja inayoelekea ukingoni.

Afisa wa Mfuko wa PSSSF Mkoani Tanga Bw.Hamidu Ally Nassoro (kulia) akimuhudumia mwanachama kwenye kampeni ya PSSSF ya mlango kwa mlango kwenye Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Mkoani humo wakati wa wiki ya huduma kwa wateja
Octoba 8,2026
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Wakati Wiki ya Huduma kwa Wateja ikielekea ukingoni, watumishi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) wameendelea kuungana na wanachama na wastaafu wa Mfuko katika kuadhimisha wiki hiyo kwa kutoa elimu na huduma mbalimbali, huku wakienda ‘extra mile’ kwa kuwatembelea wastaafu na wanachama katika baadhi ya maeneo.
Katika kuadhimisha wiki hiyo yenye lengo la kuimarisha uhusiano kati ya taasisi na wateja wake, watumishi wa PSSSF wamekuwa wakitoa elimu kuhusu huduma zinazotolewa na Mfuko, namna ya kupata huduma hizo pamoja na kuwasaidia wanachama na wastaafu kutatua changamoto mbalimbali zinazohusiana na huduma za hifadhi ya jamii.
Akizungumza kuhusu shughuli hizo, Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF, Bw. Abdul Njaidi, alisema kuwa watumishi wa Mfuko wamekuwa wakitoa huduma na elimu kwa wanachama katika ofisi za PSSSF zilizopo katika maeneo mbalimbali nchini.
Njaidi alisema hatua hiyo ni sehemu ya dhamira ya PSSSF ya kuhakikisha wanachama na wastaafu wanapata huduma kwa wakati, elimu sahihi na usaidizi unaostahili, huku akisisitiza umuhimu wa watumishi kwenda zaidi ya kutoa huduma maofisini kwa kuwafikia wateja, hususan wale wenye changamoto za kufika katika ofisi za Mfuko.
“Wiki ya Huduma kwa Wateja imetupa fursa ya kuwa karibu zaidi na wanachama na wastaafu wetu. Mbali na kutoa huduma na elimu katika ofisi zetu, watumishi wamekwenda extra mile kwa kuwafikia baadhi ya wanachama na wastaafu katika baadhi ya maeneo kama vile, Kinondoni na Kibaha mkoani Pwani.” alisema.
Alisema PSSSF itaendelea kuimarisha utoaji wa huduma unaozingatia mahitaji ya wanachama na wastaafu, kwa lengo la kuhakikisha kila mwanachama anapata huduma bora, kwa wakati na kwa ufanisi chini ya kaulimbiu ya sasa ya ‘Tunalipa Jana’.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment