RAS GEITA - WAAJIRI WASILISHENI NYARAKA NA MICHANGO KWA WAKATI ILI PSSSF "WALIPE JANA" - OKULY BLOG

Breaking

Music

Header ADS

Thursday, October 8, 2026

RAS GEITA - WAAJIRI WASILISHENI NYARAKA NA MICHANGO KWA WAKATI ILI PSSSF "WALIPE JANA"





Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Mohamed Gombati akizungumza katika semina ya PSSSF kwa maafisa Rasilimaliwatu wa mkoa wa Geita iliyofanyika mapema leo Oktoba 8, 2026 ikiwa na lengo la kuwaelimisha kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko.


Meneja wa Kanda ya Ziwa Magharibi Bw. Thomas Labi akizungumza katika semina ya PSSSF kwa maafisa Rasilimaliwatu wa Mkoa wa Geita iliyofanyika mapema Oktoba 8, 2026 ikiwa na lengo la kuwaelimisha kuhusu huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko.


Baadhi yashiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo


Baadhi yashiriki wakiwa kwenye mafunzo hayo


Washiriki wa semina ya PSSSF kwa maafisa Rasilimaliwatu na Utawala wakifuatilia mada katika semina hiyo



Baadhi yashiriki wakiwa kwenye mafunzo hayowakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi


Baadhi watumishi wa PSSSF mkoani Geita, wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi

Na Mwandishi wetu, Geita

Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Bw. Mohamed Jumanne Gombati, amewataka waajiri mkoani humo kutunza nyaraka za watumishi na kuwasilisha michango kwa usahihi na kwa wakati, ili kuuwezesha Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kutekeleza dhamira yake ya kumlipa mstaafi mara tu anapostaafu.

Akifungua semina ya PSSSF kwa wanachama na waajiri wa Mkoa wa Geita iliyofanyika Oktoba 8, 2026 katika Ukumbi wa Mikutano Otonde, Bw. Gombati alisema Wakuu wa Idara za Utumishi na Utawala, Maafisa Utumishi na Wahasibu ndio kiungo kati ya mtumishi na Mfuko. “Ninyi ni mabalozi na daraja kati ya watumishi na PSSSF. Mkitomiza wajibu wenu mtauwezesha Mfuko kutekeleza vema kaulimbiu yake ya 'Tunalipa Jana', alisisitiza.

Aidha, Bw. Gombati aliipongeza PSSSF kwa kuandaa mafunzo hayo, akisema yanaendana na msisitizo wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wake, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kutumia mifumo ya kisasa.

Aliwataka washiriki kuwahimiza wanachama na wastaafu kufuatilia taarifa zao kupitia mifumo ya kidijitali ya Mfuko.

Kwaupande wake Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa Magharibi, Bw. Thomas Labi, alisema mafanikio ya “Tunalipa Jana” yanatokana na ushirikiano wa mwanachama, mwajiri na Mfuko, na kwamba maandalizi ya kustaafu huanza siku ya kwanza ya ajira, hivyo waajiri wanapaswa kuwasajili watumishi wapya ndani ya siku 30 tangu kuajiriwa.

“Mwajiri anapohakiki madai kwa wakati, anauwezesha Mfuko kukamilisha malipo kwa wakati. Akizungumza kwaniaba ya washiriki Mkuu wa Kitengo cha Rasilimaliwatu wa Halmashauri ya Wilaya Bukombe, Bi. Caroline Kayombo, aliishukuru PSSSF kwa kuandaa mafunzo.

“Niwashukuru sana PSSSF kwa kuandaa mafunzo haya hasa namna ya kutumia mifumo ya kidigitali. Kuna mambo nilikuwa nayaelewa tofauti, lakini baada ya mafunzo haya tutaenda kufanya vizuri zaidi. Kwa niaba ya wenzangu, niwashukuru sana kwa mafunzo haya,” alisema Bi. Kayombo. PSSSF inawahimiza wanachama na wastaafu kutumia PSSSF Member Portal na PSSSF Kiganjani kufuatilia taarifa zao na wanapokuwa na changamoto kupiga simu ya bure namba 0800110055.

No comments:

Post a Comment