Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akifunga Mkutano wa Majadiliano Kuhusu Upatikanaji wa Fedha za Ufadhili wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi wa Mwaka 2026 (Tanzania Climate Finance Roundtable) chini ya kaulimbiu “Unlocking Climate Finance in the United Republic of Tanzania”, uliowakutanisha viongozi wa Serikali, washirika wa maendeleo, taasisi za fedha na sekta binafsi, uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
Na. Joseph Mahumi
Serikali ya Tanzania imesisitiza umuhimu wa kuhamisha azma ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kutoka katika mipango na ahadi kwenda kwenye uwekezaji na utekelezaji wa vitendo, ili kuhakikisha juhudi za kukabiliana na athari za tabianchi zinazaa matokeo yanayoonekana.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula, wakati akifunga Mkutano wa Majadiliano Kuhusu Upatikanaji wa Fedha za Ufadhili wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi wa Mwaka 2026 (Tanzania Climate Finance Roundtable) chini ya kaulimbiu “Unlocking Climate Finance in the United Republic of Tanzania”, uliowakutanisha viongozi wa Serikali, washirika wa maendeleo, taasisi za fedha na sekta binafsi, uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
Alisema Tanzania imeweka vipaumbele vitatu muhimu katika kuimarisha upatikanaji wa fedha za tabianchi, ambavyo ni kuimarisha mifumo ya kitaifa ya fedha za tabianchi, kuongeza mkondo wa miradi yenye ubora na inayoweza kupata uwekezaji, pamoja na kuendeleza mifumo ya kugawana vihatarishi vya uwekezaji.
“Mkutano huu umeweka msingi wa ushirikiano na mwelekeo wa pamoja katika kuhakikisha Tanzania inapata na kutumia fedha za tabianchi kwa ufanisi na kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa” alisema Mhe. Luswetula.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kanda wa Kitengo cha Planet kutoka Benki ya Dunia, Bi. Anna Wellenstein, alisisitiza umuhimu wa kujenga mkondo wa miradi yenye ubora na inayoweza kupata fedha za uwekezaji (bankable projects), kwa kuwa mabadiliko ya tabianchi ni suala muhimu kwa mustakabali wa Tanzania na ukanda kwa ujumla.
Bi. Wellenstein alisema kuwa upatikanaji wa fedha za tabianchi unahitaji maandalizi ya miradi yenye uwezo wa kuvutia uwekezaji pamoja na mifumo itakayowezesha sekta ya umma na binafsi kushirikiana katika utekelezaji wa miradi hiyo.
Naye, Kiongozi wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nchini, Bw. Nicolas Blancher alisifu mchakato wa ushirikiano unaoongozwa na Serikali, huku akihimiza washirika wa maendeleo kuoanisha juhudi zao na maeneo mahususi ya utekelezaji.
Alisema hatua hiyo itasaidia kuhakikisha makubaliano na mapendekezo yanayotokana na majadiliano yanafuatiliwa na kutekelezwa kwa ufanisi.
“Mkutano huu utumike kama jukwaa la kuimarisha na kurasimisha ushirikiano kati ya Serikali, washirika wa maendeleo na sekta binafsi katika eneo la fedha za tabianchi, huku maandalizi kuelekea Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31) yakipewa umuhimu” alisema Bw. Blancher.
Kwa ujumla, mkutano huo umehitimishwa kwa msisitizo wa kuifanya Tanzania iondoke katika hatua ya kupanga na kutoa ahadi na kuelekea katika utekelezaji wa miradi halisi ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Washiriki walieleza dhamira ya kuendelea kushirikiana katika kuongeza upatikanaji wa fedha, kujenga miradi inayoweza kupata uwekezaji na kuimarisha mifumo ya kugawana vihatarishi, hatua inayolenga kuchochea maendeleo yanayozingatia mabadiliko ya tabianchi na kuelekea uchumi unaozalisha hewa ukaa kidogo.

No comments:
Post a Comment